loader
Picha

Sekta ya mifugo yang’ara miaka minne ya JPM

MAFANIKIO ya miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli katika sekta ya mifugo yamedhihirisha kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015- 2020 kwa sekta hiyo.

Taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Utekelezaji wa Ilani hiyo kwa mwaka 2015-2019 sekta ya mifugo, iliyotolewa Septemba mwaka huu mjini Dodoma, imeeleza mafanikio yake ni pamoja na kutoa mikopo ya mifugo ya zaidi ya Sh bilioni 22.

Maeneo mengine ni kuzalisha mitamba, kuongeza malambo, majosho na visima, mafunzo kwa maofisa ugani na kuanzisha mashamba ya kuzalisha malisho kwa halmashauri 62 na kuimarisha mashamba ya kuzalisha mifugo maeneo mbalimbali.

Katika mikopo ya mifugo bora kwa wafugaji watakaojiunga katika vikundi kupitia miradi ya kopa ng’ombe/ mbuzi lipa ng’ombe/mbuzi au kopa ng’ombe/mbuzi lipa maziwa, wizara katika miaka minne imeidhinisha Sh bilioni 22 na mikopo mingine ya thamani ya Sh bilioni 11 ipo hatua mbalimbali. Kuhusu mitamba, serikali imezalisha jumla ya mitamba 51,735 katika mashamba yake na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuendelea kuizalisha kuhamasisha ufugaji wa kisasa.

“Serikali imeimarisha mashamba matano ya kuzalisha mifugo Sao Hill, Mabuki, Ngerengere, Kitulo na Nangaramo na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). Katika miaka minne mitamba 51,735 ilizalishwa mashamba ya serikali, NARCO na binafsi na kusambazwa kwa wafugaji 15,000,” ilieleza taarifa.

Katika eneo la miundombinu, serikali imeongeza malambo kutoka 1,378 hadi 1,482 sawa na ongezeko la malambo 104. Aidha malambo 301 hayafanyi kazi huku ukarabati wa lambo katika Kijiji cha Wami-Dakawa (Mvomero) ukiendelea.

“Visima virefu vimefikia 103, majosho 21 yamejengwa, 151 yamekarabatiwa na 161 yanaendelea kukarabatiwa. Minada 102 kati yake ya awali 99 na upili mitatu imeanzishwa hivyo kuongeza minada kutoka 366 iliyokuwepo mwaka 2015 hadi minada 490 kwa mwaka 2018/2019,” ilieleza taarifa hiyo.

Ilani ilielekeza eneo la miundombinu Serikali iongeze idadi ya malambo kutoka 1,378 ya sasa hadi 2,000; kujenga mabwawa katika mikoa yenye mifugo mingi; kujenga visima virefu 300.

Pia ilielekeza kujenga majosho 50 na kuanzisha minada 164 ya mifugo maeneo yote yatakayotengwa kwa ajili ya ufugaji ili kuzuia kuhamahama kwa wafugaji kunakosababisha migogoro.

Katika mashamba darasa ya uzalishaji malisho, halmashauri 62 zimeanzisha mashamba hayo yenye ukubwa wa hekta 72.5 na marobota 1,033,163 sawa na tani 22.1 za mbegu za malisho zilizalishwa mwaka 2017 hadi 2019 ikiwa utekelezaji wa Ilani.

Dodoma WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi