loader
Picha

TTCL yavuna wateja 300,000, wamo watumishi wa umma

WATUMIAJI 300,000 wa simu za mkononi wameongezeka katika mtandao wa simu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kipindi cha kuanzia Mei mwaka huu hadi sasa.

Hii ni kutokana na agizo lilitolewa na Rais John Magufuli la viongozi wote wa serikali na taasisi za umma nchini kuhakikisha kwamba wanamiliki na kutumia mtandao wa shirika hilo.

Meneja Mawasiliano wa shirika hilo, Puyo Nzalayaimisi alisema jana kuwa agizo hilo la Rais Magufuli limechangia kuongezeka kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi kwani mwitikio wa viongozi wa serikali na taasisi za umma umekuwa mkubwa.

Akizungumzia mafanikio hayo katika miaka minne, alisema ni makubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano za shirika hilo kutoka watumiaji 339,840 wa simu za mkononi Desemba 2015 hadi watumiaji 1,283,249 Septemba 2019 sawa na ongezeko la asilimia 278.

Kuhusu watumiaji wa simu za mezani alisema waliongezeka kutoka watumiaji 157,576 Desemba 2015 hadi 223,787 Septemba 2019 sawa na ongezeko la asilimia 42 hivyo kufanya watumiaji wa huduma kufikia 1,507,036 sawa na asilimia 203.

Pia limeweza kutoa gawio kwa serikali katika vipindi viwili ndani ya miaka minne ambapo kwa mara ya kwanza shirika lilitoa Sh bilioni moja na Mei mwaka huu shirika lilitoa Sh bilioni mbili kama gawio kwa serikali kwa mara ya pili.

“Mafanikio hayako katika kuongezeka wateja tu, bali hata ustawi wa shirika katika utendaji kazi kuanzia miundombinu, mazingira ya jengo lenyewe na hata ajira kwa wafanyakazi zimekuwa za kudumu tofauti na hali ya awali ambapo asilimia kubwa ya wafanyakazi walikuwa ni wa mkataba,” alisema.

Mei mwaka huu Rais Magufuli alipokuwa akipokea gawio la Sh bilioni mbili la mwaka kutoka TTCL aliagiza viongozi wa serikali na mashirika ya umma kutumia laini ya simu ya TTCL.

Dodoma WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi