loader
Picha

Simba yakwama kwa Prisons

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania bara, Simba SC jana walishindwa kuendeleza wimbi la ushindi na kujikuta wakigawana pointi dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kulazimisha suluhu katika mchezo ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Matokeo hayo yameifanya Simba kuendelea kushikilia usukani mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi tisa huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 16 katika michezo 10 iliyocheza.

Prisons inabaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mechi kwenye ligi. Katika mchezo huo uliokuwa wa aina yake kutokana na ushindani mkali ilisababisha kupatikana kadi nne za njano, tatu kwa Prisons na moja kwa Simba. Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa wenyeji Simba wakionekana kufanya mashambulizi kupitia eneo la katikati wakati wapinzani wao wakionekana kucheza mpira wakujilinda muda wote na kujibu mashambulizi kwa kushtukiza.

Hata hivyo, kadri ya muda ulivyokuwa unaenda Prisons walionekana kucheza kwa uhuru zaidi kutokana na wachezaji wengi wa Simba kuchezea mipira isiyokuwa na faida kwao na kushindwa kutengeneza nafasi ya kupata mabao.

Dakika ya 30 mchezaji, Benjamini Asukile nusura aitangulize timu yake baada ya beki wa Simba Erasto Nyoni na golikipa Aishi Manula kukosa umakini, lakini matokeo yake alipiga mpira uliotoka nje.

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alionekana kupata wakati mgumu zaidi katika mchezo huo kutokana na safu ya ulinzi ya wapinzani wao kumchunga muda wote asipate nafasi ya kufunga bao matokeo yaliyofanya hadi wanaenda mapunziko wakiwa hawajafungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kila timu ikifanya mabadiliko ya wachezaji kuongeza nguvu kutafuta ushindi wa pointi tatu, licha ya mabadiliko hayo nikama kila timu ilimsoma mwenzake kutokana na kila upande kuonekana bora.

Katika kipindi hicho Simba walionekana kuzidisha mashambulizi muda wote lakini Prisons walionekana kuwa bora kwenye safu ya ulinzi kwa kuwazuia wachezaji wa Simba wasipate nafasi ya kutengeneza mwanya wa kufunga.

Jambo ambalo walifanikiwa kuwazuia wapinzani wao hao ambao wanaonekana kuwa bora muda wote kwa kumiliki mchezo kwenye eneo la kiungo katika mchezo huo.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi