loader
Picha

Yanga, Azam FC viwanjani leo

KOCHA Charles Mkwasa leo atakuwa benchi kwa mara ya kwanza kuiongoza timu yake aliyocheza zamani Yanga ikiwa ugenini kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda.

Hiyo ni mechi ya kwanza kwa Yanga tangu ivunje benchi la ufundi lililokuwa chini ya Mwinyi Zahera, lakini pia ni mechi ya kwanza kwao tangu watupwe nje ya michuano ya kimataifa. Katika mechi ya leo, Yanga inahitaji matokeo mazuri kujindoa katika nafasi ya chini ambako mpaka sasa iko nyuma ikiwa imecheza michezo minne ina viporo vingi baada wengine kucheza michezo tisa hadi 10.

Katika michezo minne iliyocheza imeshinda miwili, sare moja na kupoteza mmoja ikiwa na pointi saba katika nafasi ya 18 ikiongozana na Ndanda iliyocheza michezo minane, ikishinda mmoja, sare nne na kupoteza mitatu.Mchezo huo huenda ukawa mgumu kwasababu timu zote mbili zinahitaji matokeo mazuri kujiondoa chini na mara nyingi Ndanda bila kujali ubora, imekuwa ikionyesha ushindani inapokutana na Yanga.

Katika michezo minane ya miaka ya karibuni waliyokutana, Yanga imeshinda minne na kutoka sare nne. Yanga itaendelea kuwakosa wachezaji majeruhi kama Lamine Moro, Paul Godfrey na Maybin Kalengo lakini bado ina wachezaji wengi wanaoweza kuibeba timu hiyo.

Mchezo mwingine ni Azam FC dhidi ya Biashara United. Tangu Kocha Aristica Cioaba apewe mikoba ya Ettiene Ndayiragije hajapata ushindi akitoka kufungwa dhidi ya Ruvu Shooting bao 1-0 na kutoka suluhu dhidi ya Kagera Sugar hivyo ana kazi ya kuhakikisha anapata ushindi.

Dodoma WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi