loader
Picha

Wasanii wajitosa kwa Mwakinyo

NYOTA wa uigizaji na muziki Esha Buheti, Steven ‘Nyerere’ Mengele na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wamezungumzia umuhimu wa mashabiki wa michezo kumuunga mkono bondia Hassan Mwakinyo kwa kujitokeza kwa wingi siku ya pambano Novemba 29, mwaka huu.

Mwakinyo anatarajiwa kuchuana vikali na bondia wa Ufilipino Arnel Tinampay katika pambano la kimataifa litakalopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Wakizungumza jana na waandishi wa habari wasanii hao walisema Mwakinyo amekuwa akipambana nje na kufanya vizuri hivyo, walitamani kumuona nyumbani namna atakavyoonyesha upinzani mkali.

Mwana FA alisema ni kitu kizuri pambano kubwa kama hilo kufanyika nchini ili kutoa fursa kwa mashabiki wa mchezo huo kushuhudia ubora wa bondia wao.

“Ngumi ni mchezo uliowekwa pembezoni lakini ni miongoni mwa michezo mizuri inayoweza kuwakilisha nchi vizuri tujitokeze kumuunga mkono Mwakinyo awakilishe vyema,”alisema.

Kwa upande wake, Esha alisema imezoeleka wanaotazama mchezo huo ni wanaume na kuhimiza mtizamo huo uondoke ili wanawake na wanaume kujitokeza kwenda kumuunga mkono Mwakinyo. Alisema alichofurahi amesikia katika moja ya mapambano ya utangulizi atakuwepo bondia mwanamke jambo lililomvutia na kuhimiza watu kwenda na wenza wao siku hiyo.

Steve Nyerere alisema haamini kama mpinzani wa Mwakinyo atafikisha raundi tano kutokana na ubora wa bondia huyo wa Tanzania na kwamba ni lazima mgeni atapike nyongo na isipokuwa hivyo basi yuko tayari kuacha sanaa.

Pambano hilo litakuwa la raundi 10 katika uzito wa kilo 69 ambapo linatarajiwa kuhudhuriwa na mgeni rasmi Rais John Magufuli iwapo kama ataridhia mwaliko kutoka kwa Promota muandaaji Jay Msangi.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi