loader
Picha

Hukumu ya Malinzi sasa Nov. 21

HUKUMU dhidi ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ((TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu iliyokuwa isomwe, imeshindwa kusomwa kwa sababu hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Maira Kasonde amehamishiwa sehemu nyingine.

Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Pendo Temu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kevin Mhina alisema kuwa hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuja kwa ajili ya hukumu jana amehamishiwa sehemu nyingine hivyo akaomba muongozo.

Hakimu Mhina baada ya kusikiliza maelezo ya wakili Temu alithibitisha kuhamishwa kwa hakimu Kasonde na kuahirisha kesi hiyo.

“Ni kweli amepata uhamisho na matayarisho yameishakamilika kumuwezesha kuandika hukumu hivyo nawapangia tarehe nyingine,” alisema Mhina.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 21, mwaka huu kwa ajili ya kusomewa hukumu. Awali kesi hiyo ilikuwa na mashtaka 30 lakini ilipofikia katika uamuzi wa kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la walipunguziwa mashtaka 10 kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili baada ya Jamhuri kushindwa kuonesha kama washtakiwa wana kesi katika makosa hayo.

Mahakama hiyo iliwakuta wana kesi ya kujibu washtakiwa hao kwa mashtaka 20 yaliyobakia baada ya Jamhuri kuonesha kwamba wana kesi hivyo walijitetea wenyewe bila kuita na mashahidi.

Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi 15 na vielelezo tisa. Katika hatua hiyo mshtakiwa watano, Miriam Zayumba aliachiwa huru kwa sababu alionekana hana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.

Washtakiwa wengine waliobakia katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 20 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Jamal Malinzi

1 Comments

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi