loader
Picha

Siwezi kuacha aina yangu ya uchezaji-Mane

MSHAMBULAIJI wa Liverpool, Sadio Mane amesema hatobadili aina yake ya uchezaji licha ya kocha Jürgen Klopp kumtetea kuhusu tuhuma za kudaiwa kujiangusha.

Mane, 27, alioneshwa kadi dakika ya 37 katika mechi ya Liverpool iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa Jumamosi iliyopita. Bosi wa Manchester Citym, Pep Guardiola kisha akazungumzia kuhusu wachezaji wa Liverpool kujiangusha ili kushinda mechi.

“Sitabadili aina yangu ya uchezaji au jinsi ninavyofanya mambo yangu,” alisema.

“Kulikuwa na makosa [dhidi ya Villa] nina hakika. Labda haikuwa penalti na haikutolewa na kunionesha kadi ya njano, niwe mkweli sina tatizo lolote na hilo.”

Bosi wa Reds Klopp alimtetea mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal baada ya kuoneshwa kadi ya njano akisema: “Sadio hana tabia ya kujiangusha kulikuwa na mazingira fulani kwenye mechi dhidi ya Aston Villa alipofanyiwa madhambi na kuanguka, labda haikuwa penalti lakini ilikuwa madhambi si kwamba aliruka mguu na kuanguka.” Mane alitania kwamba kama nafasi kama hiyo itakuja tena atajiangusha ili apate penalti.

Alisema: “Kama kujiangusha kutanipa penalti, basi nitafanya tena, kwanini nisijiangushe? Lakini alichokisema Jürgen ni sahihi, sikujiangusha.”

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: LIVERPOOL, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi