loader
Picha

Tanzania, Poland kuteta ujenzi maghala ya kuhifadhi chakula

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema serikali inafanya mazungumzo na serikali ya Poland kuona namna bora ya kumalizia ujenzi wa maghala manane ambayo walifi kia makubaliano miaka ya hivi karibuni.

Maghala hayo yataongeza uwezo wa serikali wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 250,000 hadi tani 500,000. Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili jana kuhusiana na mradi huo, Hassunga alisema Hazina ambao ndio wanaoshughulika na masuala ya fedha katika mradi huo, bado wanazungumza na watu wa Poland juu ya namna bora ya kumalizia ujenzi huo.

Mradi huo ambao ni matokeo ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Poland ya ujenzi wa maghala na uunganishaji wa matrekta Kibaha, mkoani Pwani, ulikuwa na makubaliano ya namna ya utoaji wa fedha ili kuukamilisha.

Katika makubaliano hayo kwa mujibu wa Hasunga, serikali imetoa fedha zaidi katika mradi wa matrekta na sasa mazungumzo yanaendelea namna fedha za ziada zinavyoweza kuingizwa katika mradi wa ujenzi wa maghala. Mazungumzo hayo yalitokana na kauli ya kampuni ya Feerum Spolka Akcyjna ya Poland ambayo ilisema kazi ya kukamilisha ujenzi wa maghala inasubiri serikali ya Tanzania kukamilisha malipo ya utekelezaji wake.

Mradi huo unaotekelezwa kwa ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na Poland kwa gharama ya dola za Marekani milioni 33 (Sh bilioni 76) ni kama umesimama kwa sasa.

“Tayari serikali ya Poland imeshatoa fedha hizo na utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 65 ila shughuli zimesimama hadi serikali ya Tanzania itakapotulipa fedha iliyobaki ya utekelezaji wa mradi ambayo ni dola za Marekani milioni 1.8,’’ alisema mkurugenzi mkazi wa kampuni hiyo, Mikolaj Kucia na kuongeza: “Makubaliano yalifanywa na Hazina na wao wanasema kwamba katika utekelezaji wa miradi hiyo miwili ya ujenzi na uunganishaji matrekta, fedha nyingi zimelipwa na wanafanya mazungumzo, sisi tunasubiri mazungumzo yao yakamilike ili kazi iendelee,” alisema.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Marcin Przydacz, alifanya ziara nchini na kuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Profesa Palamagamba Kabudi, ambapo mataifa hayo mawili yalikubaliana kuongeza ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Wakati wa mazungumzo na makubaliano yaliyofikiwa Septemba 20, mwaka huu, Profesa Kabudi pamoja na kuhimiza Wapolandi kuja kuwekeza nchini hasa kwenye maeneo ya uzalishaji wa dawa na kilimo hususan katika uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, uzalishaji wa mashine za viwandani na uzalishaji wa bidhaa za viwandani pia alielezea miradi mikubwa miwili ya ushirikiano. Mradi wa kwanza ni wa kiwanda cha kuunganisha matrekta kilichopo Kibaha ambao unatekelezwa kwa mkopo wa riba nafuu kutoka serikali ya Poland.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi