loader
Picha

TARI Ukirigulu yafundisha teknolojia mpya ya pamba

MAOFISA ugani 32 kutoka mikoa ya Geita na Simuyu wamefundishwa teknolojia mpya ya upandaji wa zao la pamba inayotumika nchini Brazil ili kongeza tija katika eneo hilo.

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Ukiriguru mkoani Mwanza, Robert Ngomuo alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo kuhusu zao hilo la pamba.

Ngomuo ambaye ni mtafiti wa pamba na mazao jamii ya mizizi kituoni hapo, alisema lengo ni kuwawezesha maofisa ugani hao kupeleka utaalam huo kwa wakulima kwa kuwa baada ya mafunzo hayo kila moja atatakiwa kuanzisha mashamba darasa 10 ambayo yatamilikiwa na wakulima wenyewe.

Alisema Tari Ukiliguru ipo katika hatua ya uhaulishaji wa teknolojia zinazotumika nchini Brazil ambazo zimeonyesha kuwa kwa hekta moja mkulima anaweza kupanda miche 111,000 tofauti na ilivyokuwa awali miche 55,000 tu. Alisema awali mafunzo hayo yalifanywa katika wilaya za Kwimba, Misungwi na Magu hivyo wanafikiria kwenda katika wilaya zilizopo mkoani Tabora.

“Tulifanya mafunzo haya kwa maofisa ugani wa Simiyu na Geita na kuwakusanya maofisa ugani kutoka wilaya nne ambapo tuliwachukua wanne wanne kila wilaya,” alisema.

Aliongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha maofisa ugani hao kwenda kuanzisha mashamba darasa ambayo yatamilikiwa na wakulima. Alisema teknolojia iliyokuwa inatumika ilikuwa mstari na mstari ni sentimita 90 na kati ya shimo na shimo sentimita 40 ambapo kila shimo linakuwa na mimea miwili, kwa upandaji huo idadi ya mimea inakuwa ni takribani 55 kwa hekta moja. Kwa maelezo yake nchi ya Brazil imekuwa ikitumia aina sita za upandaji ambazo ndizo zilizofundishwa kwa maofisa ugani hao

. “Moja wapo ni sentimita 60 kati ya mstari na mstari na shimo na shimo ni sentimita 30 kwa kupanda mimea miwili. “ Nyingine ni sentimita 60 mstari na mstari urefu ukiwa ni mita moja wa mlalo hapo inapandwa miche sita,” alisema.

Alisema utaalamu huo kutoka nchini Brazil unamwezesha mkulima kwenye hekta moja kupanda miche 111,000 tofauti na miche 55,000 ya awali iliyokuwa ikipandwa. Alisema upandaji huo utaongeza tija kwa wakulima kwani hivi sasa wakulima wengi wamelima eka tano lakini miche iliyopandwa ingetosha kwenye eka moja tu.

Mradi huo wa pamba ulianza mwaka 2017/18 unajulikana kama ‘Cotton Victoria Project’ umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Brazil lijulikanalo kama Brazilian Cooperation Agent (ABC) ambao upon chi tatu za Kenya, Burundi na Tanzania.

Tari Ukiliguru kwa sasa ipo kwenye hatua ya uhaulishaji wa teknolojia zinazotumika nchini Brazil. Mkurugenzi Mtendaji wa TARI, Dk. Geoffrey Mkamilo alisema taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria ya bunge namba 10 ya mwaka 2016 ikiwa na jukumu la kufanya utafiti wa kilimo.

Pia kusimamia huo utafiti wa kilimo, kuhamasisha matumizi ya teknolojia, ubunifu na mbinu bora za kilimo kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani pamoja na kuratibu shughuli zote za kilimo nchini.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi