loader
Picha

Wanafunzi waaswa kuzingatia masomo

MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila amewataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo 2019/20 kuzingatia kilichowapeleka chuoni ili wafanye vizuri katika mitihani yao na si vinginevyo.

Profesa Mwakalila alisema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa cheti, diploma na digrii kwa kuwataka wajiepushe na vitendo vyote vinavyoashiria ubaguzi, masuala ya kisasa, kuhakikisha wanakuwa na nidhamu pamoja na kuwa na matumizi mazuri ya muda ili kufikia malengo wanayokusudia. Aliwaeleza kuwa Chuo hicho kina historia iliyotukuka, kina jina kubwa, vijana wengi wanamsoma tu Baba wa Taifa kwenye vitabu lakini ni mtu muhimu kwa Taifa letu.

“ Lengo la kuzungumza na ninyi kwanza ni kuwapongeza kwa kuchaguliwa katika Chuo hiki kikongwe Cha Mwalimu Nyerere, ambacho kina historia kubwa na pia kimebeba jina Kubwa la Muasisi wa Taifa letu, kuhakikisha kile kilichowaleta hapa kitaaluma mnakifanikisha ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii na Maarifa na kumtanguliza Mungu mbele, mambo ambayo hayana msingi achaneni nayo.

“Msipoteze malengo ambayo yamewaleta hapa, mmekuja kusoma zingatieni hilo na wala msijiingize kwenye mambo ambayo yatawapotezea muda, mnapopata changamoto mbalimbali basi viongozi wa Chuo tupo na hata Serikali ya Wanafunzi ipo kwa ajili ya kusikiliza na kupatia ufumbuzi changamoto hizo,” alisema.

Alisema muasisi wa Chuo Cha Mwalimu Nyerere ni rais wa kwanza wa Taifa ambaye ni hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alianza mawazo ya kujenga Chuo kwa ajili ya wazalendo mwaka 1958 kisha chuo kufunguliwa rasmi Julai 29, 1961. alisema lengo la Chuo wakati kinaanzishwa likiwa ni kwa ajili ya kuandaa viongozi wazalendo ambao lazima waandaliwe, ili kwenda kuongoza nchi, hivyo amewahakikishia wanafunzi kuwa wapo kwenye Chuo ambacho kitawajenga kimaadili na kizalendo kwa ajili ya kuwa viongozi wazuri wa baadae.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi