loader
Picha

Kikwete ashauri SADC kupiga vita malaria

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuongeza nguvu katika vita dhidi ya malaria, kwa kuzingatia uongozi shupavu, kuwekeza fedha na teknolojia sahihi, kama njia za kuondoa ugonjwa huo Áfrika.

Kikwete alisema kasi ya mapambano imeshuka kwa sasa, hivyo jitihada hizo zinapaswa kufanyika na kukazia matumizi ya dawa mseto, vyandarua vyenye dawa na dawa ya ukoko ili kufikia asilimia 80 ya matumizi ya vyandarua, asilimia 95 ya dawa mseto, kama ilivyoamuriwa katika mikakati ya SADC.

Alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari, baada ya kuzungumza na mawaziri wa nchi za SADC wa sekta ya afya na Ukimwi katika mkutano wao, uliofanyika juzi Dar es Salaam.

Kikwete ambaye ni mmoja wa wajumbe wa jopo la watu maarufu duniani la kupambana na malaria kupitia taasisi ya End Malaria Council, chini ya uenyekiti wa bilionea Bill Gates, alisema nchi za SADC zinapaswa kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya malaria, kwa kuzingatia uongozi shupavu, fedha za mapambano na matumizi ya teknolojia sahihi.

Alisema kuondoa malaria Afrika inawezekana, ikiwa nguvu ya pamoja itawekwa. Alitoa mfano mara ya mwisho mtu kuugua malaria Marekani ilikuwa mwaka 1956, hivyo malaria kuisha Afrika inawezekana.

Alisema inasikitisha namna Afrika ilivyobeba mzigo mzito wa vifo, vinavyotokana na malaria, hivyo juhudi za kiuchumi zinazofanywa na nchi za SADC, hazitazaa matunda bila kuifuta malaria katika Afrika.

“Nimetumwa na jopo letu la kupambana na malaria kwa mawaziri hawa wa SADC, kuzungumza nao kuhusu kuongeza kasi ya kuuondoa ugonjwa huu Afrika…tunafahamu jitihada kubwa imefanyika, mafanikio yameonekana, nguvu zaidi inahitajika...mwaka 2010 hadi 2015 kulikuwa na kasi kubwa sasa imepungua, ila tunasema tusiiache. Tuweke nguvu katika mambo matatu: dawa mseto; vyandarua vyenye dawa; na dawa ukoko,” alisema Rais Kikwete.

Alisema katika maisha yake ni mtu wa matumaini, hivyo anaamini siku moja malaria Afrika itaisha. Alizitaka nchi za SADC kununua dawa za kuua viluilui vya mbu katika Kiwanda cha Viuadudu cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Kibaha mkoani Pwani katika kufanikisha juhudi hizo.

TANZANIA imeitaka Dunia na Jumuiya za Kimataifa kutambua kuwa kauli ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi