loader
Picha

Uwezo madaktari wazalendo kutibu uziwi wafikia 100%

UWEZO wa madaktari wazalendo kufanya upasuji wa masikio yenye matatizo ya kusikia nchini umefi kia asilimia 90 huku uwezo wa kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia watoto waliopandikizwa vifaa kwa watoto waliozaliwa wakiwa hawasikii ukiongezeka na kufi kia asilimia 100.

Daktari Bingwa wa Upasuaji Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila), Godlove Mfuko alisema hayo jana hospitalini hapo na kuongeza mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, hospitali hiyo ilifanyia upasuaji watoto watatu huku wengine wawili wakiwashiwa vifaa vyao waweze kusikia sauti.

Alisema jitihada za kuboresha sekta ya afya nchini, zimesaidia wataalam wazalendo kutoa huduma zao kwa ufanisi zaidi, vifaa na vifaatiba vikiimarishwa na kuongezwa. Dk Mfuko alisema tangu waanzishe huduma ya kuwekea watoto vifaa vya usikivu Juni 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), watoto 34 wamewekewa vifaa hivyo maalum vya kusaidia kusikia.

Alisema kufanyika kwa huduma hizo nchini ni mwendelezo wa wataalam hao wazalendo kuunga mkono jitihada za Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kuhakikisha wananchi wanafikiwa kwa urahisi na huduma za afya kule kule waliko.

Alisema gharama za upasuaji mgonjwa au mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha masikioni kumsaidia kusikia ni Sh milioni 36 wakati akipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayo hugharimu Sh milioni 80 hadi Sh milioni 100 mgonjwa mmoja. Alisema watoto wawili wamewekewa vifaa vya kusaidia kusikia MNH - Mloganzila na wamewashiwa vifaa hivyo waweze kusikia sauti mara ya kwanza tangu wazaliwe.

Aidha, mtoto Uebert Kigala amerekebishiwa sauti kifaa alichopandikiziwa ili kumsaidia kusikia ikiwa ni mwendelezo wa wataalam kufuatilia maendeleo yake ili kuhakikisha kifaa kinafanya kazi kwa ufanisi.

“Hawa watoto hawajawahi kusikia sauti tangu wazaliwe hivyo leo wataanza kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka baada ya kuunganisha vifaa hivi na kuviwasha’’ alisema Dk Mfuko. Dk Mfuko alitoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kupima afya zao kwa sababu asilimia 20 ya watu wenye tatizo la usikivu nchini ndio wanaoenda hospitali huku asilimia 80 wakidaiwa kubaki majumbani.

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto ameunda timu ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi