loader
Picha

Makusanyo ya kodi yazidi kupaa

KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli, makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. Mafanikio hayo yametokana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweza kukabili changamoto mbalimbali, zilizokuwa zikiikwamisha kukusanya kodi mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumzia miaka minne tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli.

Alisema katika kipindi hicho kifupi Rais ameweza kutatua kero nne kubwa. Alitaja kero hizo zilizotatuliwa na Rais Magufuli kuwa ni kudhibiti tabia ovu ya kukwepa kulipa kodi, iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kisingizio cha kufahamiana na wakubwa.

Alisema huko nyuma baadhi ya wafanyabiashara wakubwa, walikuwa wakilindwa na viongozi wakubwa serikalini hadi kufikia hatua ya kutoa maneno ya vitisho kwa watendaji wa TRA.

Lakini, tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli, tabia hiyo imekoma na kwa sasa wanalipa kama kawaida. Kayombo aliitaja kero nyingine ni kukithiri kwa matendo ya rushwa, yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA. Kwamba wahusika waliokuwa na tabia hiyo, wameshughulikiwa na sasa rushwa imepungua. Pia alibainisha kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kukabiliana na changamoto ya magendo nchini.

Alisema watendaji wa TRA walishindwa kukusanya mapato kikamilifu, kutokana na kukithiri kwa magendo yaliyokuwa yakifanywa na wafanyabiashara. Wapo wafanyabiashara waliokuwa wakipitisha mizigo kwa magendo. Mto Songwe mkoani Songwe ulikuwa na njia za magendo 32. Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, nayo yalikuwa yamekithiri kwa magendo.

Alisema tangu alipoingia madarakani, Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na njia za magendo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara, ambapo kwa sasa kuna mifumo mizuri ya ulinzi, inayozuia magendo hayo. Alisema kwa utatuzi wa kero hizo kubwa, umeenda na hamasa inayotolewa mara kwa mara na Rais Magufuli ya kulipa kodi. Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la kukusanya kodi, tofauti na huko nyuma.

Kwa sasa makusanyo yanazidi hadi Sh trilioni moja kwa mwezi. Alitoa mfano wa mwezi Septemba mwaka huu kuwa TRA ilikusanya Sh trilioni 1.768, kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kukusanywa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.

Alisema,”wananchi wanapenda kulipa kodi wenyewe bila hata ya kulazimishwa, hiyo inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali hasa afya, elimu na miundombinu za barabara. Wananchi wanaona zahanati zinajengwa, barabara zinajengwa, elimu bure, ndege zinanunuliwa, barabara za kisasa zinajengwa, ni lazima wapende kulipa kwa kuwa Rais Magufuli anakusanya kodi na inaonekana ikirejea kwa wananchi”.

SERIKALI imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi