loader
Picha

Papa Mwinyi Zahera Kaja moto kaondoka baridi Yanga

ALIYEKUWA kocha wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ni kama mlango alioingia kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho ndio mlango aliotumia kutoke ndivyo tunavyoweza kusema.

Juzi uongozi wa Yanga ulitangaza rasmi kuachana na kocha Zahera kwa sababu mbalimbali, ikiwemo timu hiyo kufanya vibaya kwenye michezo ya Ligi Kuu na ile ya kimataifa na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa timu hiyo Charles Mkwasa.

Zahera alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo na kibarua chake hicho kilipangwa kufikia tamati mwakami Septemba. Lakini hata hivyo ndoa hiyo imevunjika baada ya kocha huyo kudumu kwa kipindi cha miezi 15 tu, huku akikiongoza kikosi hicho kwenye michezo 75 ikiwa zile za kimashindano na zile za kirafiki, ambapo ameshinda 45, kufungwa 17 na sare 13.

HISTORIA YA ZAHERA

Zahera aliingia Yanga kwa stahili ya aina yake kabla ya kusaini mkataba alikuwa anakaa kwenye majukwaa kama mshabiki wa kawaida wakati uongozi wa timu hiyo ukifanya utaratibu wa kumtafutia kibao cha kufanyia kazi.

Kocha huyo alianza kazi akichukua mikoba ya George Rwandamina raia wa Zambia aliyekimbia kukinoa kikosi hicho kutokana na timu hiyo kukabiliwa na matatizo ya fedha hali iliyosababisha wachezaji kushindwa kulipwa stahiki zao kwa wakati. Makala haya yanakuletea tamu ,chungu za utawala wa kocha huyo alipokuwa anakinoa kikosi hicho kwa kipindi hicho cha miezi 15:-

TAMU ZA ZAHERA

Timu hiyo katika msimu wake wa kwanza ikiwa na Zahera, ilimaliza ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya ukata mkali uliokuwa ukiikabili timu hiyo. Simba ilitwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo. Pamoja na hali hiyo ngumu bado kocha huyo alimwagiwa sifa na kwa stahili yake ya kiuzalendo pale alipokuwa akiwachangisha mashabiki wa timu hiyo kila walipofika kushuhusia mechi za timu yao hiyo.

USAJILI WAO

Usajili uliofanywa na Yanga msimu huu ulisimamiwa na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Mwinyi Zahera na walifanikiwa kufanya hilo mapema ingawa ni jambo ambalo halikuwai kufanyika kwenye timu hiyo kutokana na utamaduni waliojiwekea kwa kila kiongozi kusajili wachezaji wake na kuwapelekwa katika klabu. Usajili huo ulikuwa mkubwa na kwa asilimia kubwa wachezaji wengi wanaunda kikosi cha mabingwa hao wakihistoria ni wachezaji wapya jambo ambalo lilifurahiwa na mashabiki wengi wakizidi kuamini kwamba timu hiyo itakuwa moto kuotea mbali kwa kuanza Ligi kwa kishindo.

KUSHIRIKI KIMATAIFA

Taarifa za njema za kurejea kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa zilifika wakati timu hiyo kwa asilimia kubwa imeshafanya usajili wa kikosi chake, huku huku wakiwa wamebakiza nafasi za wachezaji wachache ambao walikuwa wanamalizia mazungumzo ya mwisho.

Ujio wa taarifa hiyo ya Tanzania kuingiza timu nne, mbili za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na mbili Kombe la Shirikisho na Yanga kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika. Pamoja na kupata nafasi hiyo kwa bahati ya mtende iliyochangiwa kwa asilimia kubwa na watani zao Simba baada ya kufanye kweli kimataifa kwa kutinga hadi hatua ya robo fainali,kuliangana na usajili walioufanya waliamini kwamba bado kikosi chao kinauwezo wa kufanya kweli.

KAZI ZAIDI YA KOCHA

Kwa nyakati tofauti alikuwa kama mzazi au mdhamini wa timu hiyo kwani alikua atoa fedha zake mfukoni kugharimia chakula cha wachezaji ili mambo yaende au wakati mwingine ndio alikuwa akiwaamasisha mashabiki kuichangia Yanga. Aidha, alikuwa anajitolea kupita kuchangisha fedha kwa mashabiki ikiwemo kupita kuzunguka kwenye vyombo vya habari kuwaomba mashabiki kuichangia timu hiyo ipate kujiendesha.

CHUNGU ZA ZAHERA

Pamoja na mashabiki wa timu hiyo kuamini kikosi chao kuanza msimu vyema, lakini mambo yamekuwa tofauti baada ya kikosi hicho kuanza Ligi kwa kusuasua, ambapo hadi sasa wemecheza mechi nne wakishinda mechi mbili na kutoka sare moja na kupoteza.

Kupoteza pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting ni moja ya kitu kilichoibua minong’ono mikubwa kwa kuwa timu hiyo ilitoka kucheza michezo ya kimataifa na ilikuwa inafanya vizuri, lakini kiwango kilichooneshwa na wachezaji wa timu hiyo hakikuwafurahisha kabisa. Ruvu Shooting ni miongoni mwa timu ambazo hazikuwa na rekodi ya kupata ushindi mbele ya Yanga, lakini msimu huu ilikuwa tofauti kwani waliibuka na ushindi wa 1-0.

KAULI ZAKE TATA

Kwa mfano: “Mashabiki wa Yanga wanaipenda Yanga kushinda wanawake wao, “kikosi changu hakina uwezo wa kuifunga Pyramids.” Zahera amekuwa nimiongoni makocha ambao wana kauli tata ambazo zilikuwa zinahibua hali ya sintofahamu kwa mashabiki wa timu hususani baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Pyramids kwa mabao 2-1 alisema kikosi hicho kilistahili kupata matokeo hayo . Kwa kuwa wachezaji waliosajili hawana uwezo wakushindana kwenye michezo ya kimataifa na kwamba wachezaji wake walisajiliwa kwa ajili ya ligi ya ndani.

MASHABIKI KUMCHOKA

Baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Pyramids kwa kupoteza kwa mabao 2-1 mashabiki wa timu hiyo walimrushia chupa za maji kushinikiza kocha huyo afutwe kazi na kwamba katika mchezo huo walikuwa wanahitaji zaidi matokeo mazuri. Lakini badala ya kushinda, timu hiyo ilifungwa 2-1 tena na timu ambayo ilikuwa inaonekana kama inaweza kufungika kutokana na kiwango chake, tofauti kabisa na timu zingine za Misri, ambazo ziko juu zaidi.

SERIKALI imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi