loader
Picha

Mkwasa arudisha shangwe Yanga

KOCHA wa muda wa Yanga, Charles Mkwasa amerejesha shangwe klabuni hapo baada ya jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Ugenini Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Mkwasa jana alikiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza na kupata ushindi huo huku timu ikionekana kucheza kwa ari kubwa. Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga alipewa mikoba hiyo katikati ya wiki hii baada ya uongozi kuachana na kocha Mwinyi Zahera kwa kushindwa kuivusha timu kwenye michuano ya kimataifa.

Patrick Sibomana ndiye alikuwa shujaa wa Yanga jana akifunga bao la ushindi dakika ya 75 kwa mpira wa adhabu iliyotolewa na mwamuzi Hans Mabena wa Tanga baada ya mchezaji wa Ndanda kushika mpira. Mwamuzi Mabena alilazimika kuamrisha adhabu hiyo ipigwe tena baada ya ile ya kwanza kukosewa kutokana na wachezaji wa Ndanda kuwahi kutoka kabla mpira haujapigwa.

Katika mchezo huo wa jana, Yanga ilionekana kuwa na udhaifu eneo la viungo hasa baada ya kushindwa kutengeneza nafasi za kutosha na kutumia muda mwingi kucheza mipira ya pembeni ambayo wapinzani wao walikuwa imara katika maeneo hayo. Yanga ilitengeneza nafasi tatu pekee ambazo hazikuzaa matunda baada ya David Molinga kushindwa kutumia nafasi ya wazi iliyotengenezwa na kiungo wa pembeni Mapinduzi Balama, wakati nafasi zingine mbili zikipotezwa na Sibomana.

Kwa upande wa wapinzani wao Ndanda walikuwa bora zaidi katika sehemu ya kiungo ambayo kwa kiasi kikubwa ilimiliki mpira licha ya kwamba walishindwa kutengeneza nafasi za kutosha huku washambuliaji wao wakishindwa kutumia maarifa ya kuivuka ngome ya Yanga.Kipindi cha pili kilianza huku mshambuliaji wa Yanga Sibomana akiwa anaongoza kwa kuwa na mashuti matatu ambayo yote hayakulenga lango la wapinzani wao.

Wakati timu hizo zikiendelea kushambuliana Ndanda ilifanya mabadiliko dakika ya 64 ambapo alitoka Hussein Javu na kuingia Nassoro Saleh, hata hivyo mabadiliko hayakuwa na tija.

Dakika mbili baadaye Yanga ilijibu mapigo hayo baada ya kufanya mabadiliko ya kumtoa Rafael Daudi na kuingia Mrisho Ngassa ambaye aliongeza kasi ya mashambulizi na Ndanda kuanza kucheza faulo muda wote jambo lililowagharimu na kusababisha bao.

Kama ilivyo kawaida kwa kampuni ya GSM, baada ya ushindi huo Yanga itapewa zawadi ya Sh milioni 10 kama sehemu ya kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo ambao wamekuwa na kipindi kigumu katika michezo ya hivi karibuni. Matokeo mengine ya michezo ya jana KMC ikiwa katika Uwanja wa Uhuru ilipoteza mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi