loader
Picha

Aussems akiri Prisons waliwazidi

KOCHA wa timu ya Simba SC, Patrick Aussems amekiri suluhu iliyopata timu yake dhidi ya Prisons juzi ilitokana na wachezaji wake kuzidiwa. Mabingwa hao watetezi walibanwa na Prisons na kutoka suluhu katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam juzi.

Akizungumza baada ya mechi hiyo juzi, kocha huyo mbelgiji alisema wapinzani wao walicheza mpira wa kujilinda muda wote na kutumia nguvu kupokonya mipira jambo lilowafanya wachezaji wake kukosa ufanisi wa kutengeneza nafasi pamoja na kumiliki mpira muda mwingi. Aussems alisema licha ya matokeo hayo sio mazuri kwao baada ya kushindwa kutimiza malengo ya kuondoka na pointi tatu lakini hawana budi kuwaheshimu wapinzani wao kwa kucheza mchezo ambao walitarajiwa kupata matokeo kama hayo.

“Wachezaji wangu walizidiwa kwenye nguvu na kasi ya mchezo kutokana na nguvu kubwa iliyotumiwa na wapinzani wetu kwa kiasi kikubwa wamechangia kutuharibia malengo yetu ya kutoka na pointi tatu,” alisema Aussems.

Aidha, alisema matokeo hayo hayamfanyi kukata tabaa ya kutetea ubingwa wao kwani bado wanaongoza ligi hivyo wanaenda kujipanga upya kwa mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu kwenye uwanja huohuo. Kwa upande wake kocha wa Prisons, Adolf Richard alisema wachezaji wake kucheza kwa nidhamu na kuwaheshimu Simba kwa kujilinda wakati wote kuliwafanya kutoka na pointi moja waliyoitarajia.

Prisons inabaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mechi kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi hiyo. Aidha kwa upande wake alikiri Simba ni miongoni mwa timu iliyowapa wakati mgumu kupata matokeo kulingana na ubora walionao wachezaji wake wengi wanaounda kikosi hicho.

“Simba ni timu bora inawachezaji saba timu ya taifa, tuliingia tukiwa na lengo moja kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza tumefanikiwa kimbinu tumetoka na pointi moja kwetu ni kubwa kulingana na ubora wa timu tuliyocheza nayo,” alisema Richard

SERIKALI imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi