loader
Picha

Ibrahimovic kurudi AC Milan

ZLATAN Ibrahimovic anajiandaa kurejea AC Milan atakapomaliza mkataba wake na LA Galaxy, kwa mujibu wa msimamizi wa Ligi ya Marekani Don Garber. Mshambuliaji huyo wa Sweden alijiunga na klabu hiyo ya Los Angeles Machi 2018 lakini mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

“Zlatan ni mchezaji anayevutia,” Garber aliiambia ESPN.

“Anakupa unachotaka ndani ya dakika.”

“Ni mchezaji mwenye umri wa miaka 38 aliyetengenezwa na AC Milan, moja ya klabu kubwa duniani.”

Ibrahimovic alicheza kwa miamba hiyo ya Serie A Milan kati ya mwaka 2010 na 2012, na kufunga mabao 42 katika mechi 61 za ligi alizocheza.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Sweden mechi za karibuni alizoichezea LA Galaxy ilikuwa ni ile waliyofungwa 5-3 na Los Angeles FC kwenye kombe la ligi. Ibrahimovic amefunga mabao 53 akiwa Marekani na alichaguliwa kwenye timu bora ya ligi ya Marekani msimu wa mwaka 2018 na 2019.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: LOS ANGELES, Marekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi