loader
Picha

Msemaji wa serikali ampongeza Nandy

MSEMAJI Mkuu wa Serikali DK.Hassan Abbas amempongeza msanii wa muziki wa Bongo Fleva Faustina Mfi nanga ‘Nandy ‘ kwa kuimba wimbo unaomsifu rais John Magufuli kutokana na juhudi zake katika utendaji kazi.

Juzi msanii Nandy aliachia video ya wimbo huo unaoitwa Magufuli ambao amebadilisha maudhui kutoka katika wimbo wake wa Ninogeshe alioimba mwaka mmoja uliopita. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, msemaji huyo wa serikali alisema kazi ya sanaa ni kuonesha palipo na kasoro na kuonyesha mema kwa faida ya jamii kwa kuliona hilo aliamua kumpongeza msanii huyo.

“Kazi ya sanaa ni kuonesha kasoro na palipo na jema kwa faida ya jamii nzima, natumia fursa hii kumpongeza msanii Nandy katika video yake ya rais Magufuli,”alisema Abbas.

Baada ya msanii huyo kuona pongezi hizo hakusita kutoa shukran zake kwa msemaji huyo kwa kumwambia “asante sana msemaji mkuu wa serikali,”.

Imekuwa ni mwendelezo kwa wasanii wa muziki kutambua juhudi kubwa za rais Magufuli kwani hata msanii Rajab Abdul ‘Harmonize’ aliimba wimbo wa kusifu juhudi za rais.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi