loader
Picha

Nditiye: Mvuto si kigezo cha kuajiri wafanyakazi ATCL

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema serikali haitumii kigezo cha mvuto katika kuajiri watumishi wa Shirika la Ndege nchini (ATCL).

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima kutaka shirika hilo liajiri wahudumu wenye mvuto ili kufanya shirika hilo kuonekana.

“Naomba nitoe ufafanuzi wa jambo ambalo lilisemwa bungeni jana (juzi) ni kuwa ajira za shirika la ndege haziangalii mvuto.”smesema Nditiye.

Amesema serikali na shirika hilo vimeainisha sifa mbalimbali za kuajiri, ikiwa ni pamoja na kuwa Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.

“Pia awe anayefahamu lugha za Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha na awe na cheti cha kuongoza ndege ama cha kufanya kazi ndani ya ndege. Sifa muhimu ni lazima awe na leseni ya kuruka ambayo inatolewa na Mamlaka ya Anga (TCAA),” alisema.

Nditiye alitaja sifa nyingine za ziada ni kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali ya kitaifa, kidunia, utalii na kuongeza pia anatakiwa kuwa na hekima, heshima, maadili na kwamba watamchunguza kama anafaa kuajiriwa.

“Sifa nyingine zote zinazozungumzwa si sifa zinazozingatiwa na ATCL wala serikali yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Katika swali la msingi, Mbunge wa Igalula, Mussa Ntimizi (CCM), alisema,

“wananchi wa Kata ya Tura katika Vijiji vya Mwamlela, Mmunyu na Ikongwa hawana kabisa mawasiliano ya simu, licha ya umuhimu wa mawasiliano kiusalama na kiuchumi. Ntimizi alitaka kujua serikali inatoa ahadi gani ya kupatikana kwa mawasiliano katika vijiji hivyo.

Akijibu swali hilo, Nditiye alisema serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma za mawasiliano kote nchini.

Alisema kuwa Julai mwaka huu mfuko ulitangaza zabuni ya awamu ya nne kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 521 zenye vijiji 1,222. Nditiye alisema kuwa kata ya Tura ilijumuishwa kwenye zabuni, ikiwa na vijiji vya Karangasi, Mmunyu na Mwamlela na kwamba ilifunguliwa na baada ya tathmini, kupata mzabuni katika maeneo haya. Utekelezaji utaanza baada ya mkataba kusainiwa mwezi Desemba mwaka huu.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi