loader
Picha

Uswisi yarudisha thamani ya sanaa nchini

SANAA na utamaduni ni moja ya nyenzo muhimu zinazovutia katika kuwasilisha mawazo kwa jamii kwa njia ya uigizaji wa majukwaani, uchoraji, uchongaji, ngoma na muziki.

Kwenye makongamano makubwa ya sanaa watu wamebuni mbinu zinazoweza kufikisha ujumbe kwa watu kiurahisi ni kuweka vikundi vya sanaa za maonesho ya majukwaani ambapo huigiza mada husika na hata kuimba kwa ngoma kisha wadau wanaibua mjadala. Njia hiyo hakika imesaidia kuwavuta watu karibu na kusikiliza kwa makini ni kitu gani hasa kinazungumzwa kisha watu wanajadili jambo linaloweza kufanyika ili kuleta muafaka wenye manufaa kwa jamii.

USWISI NA SANAA

Moja ya balozi zilizojitahidi kuipa thamani sanaa katika utoaji elimu kwa jamii ni Uswisi chini ya Balozi aliyemaliza muda wake, Florence Mattli. Wapo wasiotambua thamani yake lakini pia, wapo wanaoelewa nguvu yake katika kufikisha ujumbe na miongoni mwao ambao wamekuwa mstari wa mbele ni Ubalozi huo wa Uswisi Tanzania na Zambia.

Uswisi ni miongoni mwa balozi zilizowabeba wasanii kupitia miradi yao kadhaa ya kijamii waliyoanzisha ndani ya miaka mitatu na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafikia walengwa kwenye mikoa mbalimbali nchini kutokana na jinsi inavyowasilishwa.

Gazeti hili lilifanya mazungumzo na Mshauri wa Ubalozi wa Uswisi Tanzania na Zambia hapa nchini Eliachim Malimi anayesema wanaipa thamani kubwa sanaa katika kufikisha ujumbe kwa sababu ina nguvu ya kuwafikia watu kwa haraka.

“Tangu tuanzishe miradi mitatu iliyopita ikiwemo suala la rushwa, mimba za utotoni na mazingira kwa kuwashirikisha wasanii tumeona nguvu kwa jamii, wananchi wamepata uelewa haraka, wamejifunza na hata vijana wengi wamejifunza kile kilichohitajika kwao,” anasema.

Malimi anasema mradi wao wa kwanza ulihusu rushwa ambapo waliita wasanii kuandika maombi yao na kueleza ni kwa vipi wakipewa pesa watazitumiaje katika kusaidia kuelimisha na kupunguza vitendo hivyo kwa jamii.

Anasema mradi huo haukubagua ni msanii wa aina gani ilimradi kuandaa muswada unaovutia kuelimisha kupitia sanaa zao na watu wakaelimisha na kupunguza tatizo lililopo. Anasema zaidi ya wasanii 200 waliomba lakini wale waliokidhi vigezo walichaguliwa na kupewa fedha ambapo zaidi ya Sh milioni 190 zilitolewa katika mradi huo wa kupunguza vitendo vya rushwa kupitia sanaa lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na vitendo hivyo.

“Baadhi ya wasanii walionufaika walitoka Makumbusho ya Taifa, nyumba ya vipaji vya sanaa (THT) kwa kushirikiana na Clouds Media, Sanaa Tanzania, Gaba Afrika na Kijiji studio kwa kushirikiana na Nafasi art space,” anasema.

Mshauri huyo anafafanua kuwa wasanii hao walikwenda mikoa mbalimbali na bado walishirikisha makundi mengine ya wasanii kwenye mikoa waliyokwenda kama Mtwara, Shinyanga na kwingine waliopewa elimu ili nao kushiriki kikamilifu kutoa mafunzo kwa wengine. Mradi mwingine ulikuwa unahusu mimba za utotoni ambapo pia anasema vijana wengi walipewa elimu kupitia sanaa ya uigizaji na muziki.

Anasema baadhi ya wasanii waliopata fedha za mradi huo walikwenda katika mikoa iliyoathiriwa zaidi kama Shinyanga, Mara na waliandaliwa michoro ya katuni kupata elimu. Kupitia mradi huo wasanii walipewa zaidi ya Sh milioni 215 huku ujumbe wake ukisema wawezeshe vijana wa kike kwa njia ya sanaa. Mradi huo ulitolewa mwaka jana na bado makumbusho ya taifa walishiriki kwa mara nyingine kuomba na kufanikiwa kupata fedha sambamba na wasanii Paulo Gomez kwa kushirikiana na Pili Maguzo, Gaba Afrika Limited na Nafasi, na Sahara and Faru.

Na mwaka huu walizindua mradi ambao unahusisha mazingira, kuzigeuza taka kuwa bidhaa muhimu na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake Florence Mattli alionekana kuridhika na utekelezaji wa miradi iliyopitia sanaa.

VIKUNDI VYAFAIDIKA

Kwa mujibu wa Malimi, vikundi vitano vya sanaa walinufaika na zaidi ya Sh milioni 174 na Makumbusho ikiwa ni miongoni mwa waliovuna pesa baada ya kufanya vizuri katika miradi mingine iliyopita. Makumbusho wamekuwa wakihusika kwa kiasi kikubwa na sanaa ndio maana waliweza kunuifaka kwa miradi mbalimbali.

Mbali na hao, wengine walionufaika ni Chuma art wamekuwa wakiokota vyuma chakavu na chupa na kutengeneza mapambo ya nyumbani kama wanyama, wadudu na tena ni wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa kuwashirikisha watu wenye ulemavu.

Chini ya mradi huo, Chuma art ilifanikiwa kutengeneza pia, mjusi mkubwa kwa kutumia vyuma chakavu na amewekwa kwenye jumba la makumbusho na sasa ni kivutio kikubwa kwa watalii wanaokwenda kutembelea eneo hilo. Ukiachilia mbali watu wa Chuma, wengine walionufaika ni Alama arts and Media Production, Fourteen Plus, na kikundi cha sanaa na maendeleo Afrika Mashariki (CDEA).

Wote hao ni wale waliochangia fursa baada ya kutolewa matangazo kuwa waombe pesa na kulenga kitu gani. Miradi hiyo hakika imewasaidia wasanii sio tu kutoa elimu kama walivyoelekezwa bali kujiongezea kipato. Anasema miradi hiyo inatarajiwa kuhitimishwa mwishoni mwa mwaka huu na huenda sasa fursa nyingine zikatangazwa baadaye ili kuendeleza utamaduni wao wa kuelimisha jamii masuala mbalimbali kupitia sanaa.

CHANGAMOTO

Malimi anasema baadhi ya wasanii wanashindwa kuchangamkia fursa kama hizo kwa kukosa uelewa kutokana na asilimia kubwa ya waliopo kwenye vikundi kutokuwa na elimu na wengine hawajui wafanye nini.

Anawahimiza umuhimu wa kujiendeleza kielimu ili iwasaidie katika harakati za kukuza sanaa hiyo nchini na hata zinapotokea fursa basi inakuwa ni rahisi kwao kuomba. art ilifanikiwa kutengeneza pia, mjusi mkubwa kwa kutumia vyuma chakavu na amewekwa kwenye jumba la makumbusho na sasa ni kivutio kikubwa kwa watalii wanaokwenda kutembelea eneo hilo. Ukiachilia mbali watu wa Chuma, wengine walionufaika ni Alama arts and Media Production, Fourteen Plus, na kikundi cha sanaa na maendeleo Afrika Mashariki (CDEA).

Wote hao ni wale waliochangia fursa baada ya kutolewa matangazo kuwa waombe pesa na kulenga kitu gani. Miradi hiyo hakika imewasaidia wasanii sio tu kutoa elimu kama walivyoelekezwa bali kujiongezea kipato. Anasema miradi hiyo inatarajiwa kuhitimishwa mwishoni mwa mwaka kuridhika na utekelezaji wa miradi iliyopitia sanaa.

VIKUNDI VYAFAIDIKA

Kwa mujibu wa Malimi, vikundi vitano vya sanaa walinufaika na zaidi ya Sh milioni 174 na Makumbusho ikiwa ni miongoni mwa waliovuna pesa baada ya kufanya vizuri katika miradi mingine iliyopita. Makumbusho wamekuwa wakihusika kwa kiasi kikubwa na sanaa ndio maana waliweza kunuifaka kwa miradi mbalimbali. Mbali na hao, wengine walionufaika ni Chuma art wamekuwa wakiokota vyuma chakavu na chupa na kutengeneza mapambo ya nyumbani kama wanyama,

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi