loader
Picha

Washauriwa kulima kahawa bila kemikali

WAFANYABIASHARA kutoka Uingereza na Afrika Kusini wanaojihusisha na biashara ya kahawa hai inayolimwa bila kemikali, wamesema mahitaji yake ni makubwa duniani na kutaka Watanzania kujikita katika kilimo hicho ili kujipatia mapato.

Walibainisha hayo mjini hapa walipotembelea mashamba ya kilimo hai yaliyopo Shimbwe Juu, kata ya Uru kwa ajili ya kutafuta kahawa hiyo ili kukamilisha hitaji lao la kontena kubwa 16 huku wakiwa wamepata kontena nane pekee Rungwe mkoani Mbeya. Mmoja wa wafanyabiashara hao, Paul Cooker wa kampuni ya CTCS ya Uingereza alisema kutokana na mahitaji yaliyopo walifika kutafuta tani 16 za kahawa hizo hai kutoka nchini lakini wamepata kontena hizo nane kutoka Rungwe mkoani Mbeya.

“Tumekuja huku sasa kuangalia ikiwa tutapata zilizobaki kwani mahitaji ni makubwa na kahawa ya nchi hii hupendwa sana,” alisema na kuongeza kuwa mahitaji ya kahawa inayolimwa kwa njia za asili ni makubwa na bei yake ni kubwa tofauti na inayolimwa kwa kutumia kemikali kwani kahawa hai ni tiba katika kuondoa msongo wa mawazo na maumivu ya kichwa.

Mfanyabiashara kutoka Afrika Kusini wa kampuni ya Tribeca Cofee, Mart Carter, alisema mazingira ya mashamba ya asili yanapendeza huku yakitoa mazao bora ambayo ni muhimu kwa afya.

Aliwataka wananchi kujikita katika kilimo hicho ili ‘kukamata’ soko kubwa lililopo. Mkulima wa eneo hilo, Remmy Temba alisema katika shamba alilorithi kutoka kwa baba yake mwaka 1979 amekuwa mkulima wa shamba hilo la asili na kwamba hatumii kemikali na mbolea kukuza mazao.

“Ukiangalia hapa shambani kwangu nina mazao mchanganyiko, matunda na mboga hivyo kusaidia udongo kuendelea kuwa na rutuba na mifugo niliyonayo kuku, mbuzi na nguruwe hunipatia mbolea za asili,” alisema.

Alisema shamba hilo la ekari tatu linamuwezesha kupata mazao ya asili kwa matumizi ya nyumbani na kuwa na afya njema huku akisomesha watoto wake saba katika hatua ya vyuo vikuu na wawili wakiwa sekondari.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko, Moshi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi