loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hakirasilimali watoa neno Tanzania ya viwanda

MTANDAO wa Hakirasilimali umesema kuendeleza ubia kati ya Serikali na wadau na kuzingatia matakwa ya wananchi ni mambo ya msingi kuiwezesha Tanzania kutimiza lengo na kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Rachael Chagonja ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Habarileo nje ya Jukwaa la Tisa la Uziduaji lililofungwa Alhamisi wiki hii.

Jukwaa hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Asasi za Kiraia (Azaki) 2019 iliyoanza Novemba nne hadi nane.

“Kuendeleza ubia huo kunakuja wa njia tofauti, wanaweza wakafanya kazi na timu za tafiti, timu ya wataalamu wanaweza kufanya utafiti wa kutosha wakapembua yale ambayo yanahitajika na kuishauri Serikali” amesema kiongozi huyo wa Hakirasilimali.

Hakirasilimali ni mtandao wa asasi za kiraia unaofanya kazi katika sekta za madini, mafuta na gesi.

“Lakini pia tujifunze kujifunza kutoka kwa wengine nchi ambazo tayari zilishaendelea. Tujifunze tujue changamoto zao zilikuwa ni nini na namna gani sisi kama nchi tunaweza tukazikabili zile changamto ambazo wao walipitia katika nchi husika. Kwa hiyo vipaumbele viendane pia na matakwa ya wananchi isiwe tu kitu ambacho kinaendelea katika level ya juu, pia hiyo vision iwe inclusive ndio maana nikasema tujenge dhana ya kuwa na ubia”amesema Rachael.

Wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Hakirasilimali, Donald Kassongi alisema, mapinduzi ya nne ya uchumi yanahitaji teknolojia na ubunifu hivyo ni muhimu Serikali naa wadau wafanye kazi pamoja ili pia kujenga dhana ya kuaminiana.

“Pengine teknolojia tunaweza tukanunua lakini ubunifu tunahitaji kuujenga na tuwe tayari kuja pamoja. Serikali inazo rasilimali watu na rasilimali nyingine na inaweza kushirikiana na kujifunza mahali pengine lakini asasi za kiraia pia zinawekeza katika kujenga uwezo kutoka kwenye jamii kwa sababu dhana kubwa ya asasi za kiraia ni kuleta yale ambayo yamekuwepo kwenye jamii na kuyapeleka panapohusika” amesema Kassongi.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

1 Comments

  • avatar
    BUNDALA CHARLES
    10/11/2019

    Comment namushukuru sana rais magufuli kwa juhudi anazofanya. namtakia maisha mema.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi