loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Liverpool yaicharaza Man City bao 3-1

USHINDI wa Liverpool wa mbao 3-1dhidi ya Manchester City umezidi kuwaongezea kasi majogoo hao wa Anfield  ambao mpaka sasa wanaongoza Ligi Kuu England wakiwa na pointi 34 baada ya kucheza michezo 12.

Mabao ya kiungo Fábio Tavares ‘Fabinho’ dakika ya sita, pamoja na yale ya washambuliaji Mohamed Salah (dakika ya 13) na Sadio Mane (dakika ya 51) yalitosha kuipa Liverpool ushindi huku Manchester City wakipata bao la kufuta machozi mnamo dakika ya 78 kupitia kwa Bernado Silva.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kuendelea kubaki kileleni wakiwa wamefikisha pointi 34, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Leicester City wenye pointi 26 wakati nafasi ya tatu ikiwa kwa vijana wa Chelsea wenye pointi 26. Nafasi ya nne inashikiliwa na Manchester City wenye pointi 25 (tisa nyuma ya Liverpool )

Katika mchezo huo, Liverpool walitawala kipindi cha kwanza, huku Manchester City wakitawala kipindi cha pili cha mchezo huo ambapo waliweza kupata bao la kufutia machozi.

LIVERPOOL (4-3-3): Alisson; Alexander-Arnold , Lovren, Van Dijk, Robertson;

Fabinho, Wijnaldum, Henderson (Milner dk 61); Mane, Firmino(Chamberlain dk 79);, Salah (Gomez dk 87);

Manchester City (4-3-3): Bravo, Walker, Fernandinho, Stones, Angelino; Gundogan, De Bruyne, Rodri; B Silva, Aguero (Jesus dk71), Sterling.

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: LIVERPOOL, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi