loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yatoa tril 1.9/- kuwezesha wananchi

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Antony Mavunde amesema serikali itaendelea kuunga mkono shughuli za maendeleo zinazofanywa na wanawake.

Alisema hayo mjini Dodoma wakati wa hafla ya jioni iliyoandaliwa na Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) na kushirikisha wabunge.

Mavunde alisema serikali imekua ikifanya juhudi mbalimbali ikiwemo kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kuweza kuendeleza miradi na biashara mbalimbali wanazofanya.

Mavunde ambaye pia ni mbunge wa Dodoma Mjini alisema serikali imeshatoa zaidi ya Sh trilioni 1.9 kupitia mifuko yake 19 ya kuwezesha wananchi na wengi wamebadilisha maisha kupitia mifuko hiyo.

Alisema ni wakati sasa wa kuhamasisha wanawake kuja kufanya uwekezaji Dodoma kwani ni sehemu inayounganisha mikoa mingi na miundombinu inaboresha.

Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya IBRA Contractors, alisema VoWET wana jukumu la kuwafikia wanawake Tanzania na anaamini wana uwezo wa kuondoa umaskini kwa kasi zaidi.

Alisema asilimia 51 ya viwanda vidogo vinaendeshwa na wanawake na wanalipa kodi bila shuruti.

“VoWET tunataka wanawake wafanye biashara katika sekta zote kenye uchimbaji madini, gesi katika mapambano ya kuinua mwanamke kujiinua kiuchumi tumejikita katika kupaza sauti, kushawishi wanawake kurashimisha biashara zao, kutoa elimu na utetezi kwenye mazingira ya biashara kwa kuangalia sera na sheria,”amesema.

Amesema VoWET imeanzisha Sacoss na kupitia taasisi hiyo wameweza kukopesha zaidi ya Sh milioni 700 na kila mwanachama amenunua kiwanja Dodoma.

Pia alisema kuna changamoto kubwa ya wanawake kutokopoesheka na kuiomba serikali na wadau wa maendeleo wanzishe Mfuko wa Wajasiriamali Wanawake ambao utasaidia kukopesha wanaopata zabuni mbalimbali.

Mbunge wa viti Maalum, Amina Mollel alisema biashara ni mtandao, wanawake wajitambue wasiogope kukopa kwani fedha zipo.

Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Rama Makani alisema juhudi za wanawake kujiinua kiuchumi zinatakiwa kuungwa mkono.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamisi akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, alisema serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuwawezesha wanawake kiuchumi.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi