loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi msingi, sekondari hatarini kupata VVU

WASICHANA na wavulana anaoingia kwenye mapenzi wakiwa na umri mdogo wametakiwa kuacha mchezo huo, kwani wanajiweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa wenzao.

Imeelezwa kuwa vijana wadogo wengi katika shule za msingi na sekondari wamekuwa wakifanya mapenzi na watoto wenzao na wapo miongoni mwao ambao wamezaliwa na virusi hivyo na wanaweza kuambukizana.

Hayo yamesemwa na Mshauri Kiongozi wa mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS), Ally Kebby wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Actions Girls (AGF) ambayo inafanya kazi ka kushirikiana na serikali kutoa elimu ya afya ya uzazi na haki kwa vijana.

Kebby alisema kuna watoto wanaozaliwa na virusi vya Ukimwi na wako shule za msingi na sekondari na ni muhimu pia kama taifa kuanza kuangalia suala la maambukizi ya Ukimwi kupitia makundi hayo.

“Tuna uhakika wanafunzi hao hawafanyi ngono na wenzao? tunashughulikia na hilo tatizo kwa wakati gani, maana wapo lakini hawataki kuonekana kuwa wana tatizo,” alisema na kuongeza kuwa suala hilo mtu anapotaka kulizungumza anaonekana kama anaanza unyanyapaa kwa makundi ya watoto.

Hata hivyo alisema ni lazima jamii ijue tatizo hilo kwani wanafunzi hao wanajijua na wako kwenye programu ya kuchukua dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) lakini hawataki kujulikana.

Alisema ni wakati sasa wa suala hilo kuangaliwa ili kuona wanaishi salama bila kuambukiza wenzao. Kwa upande wake, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Action Girls Foundation (AGF), Rabia Mussa alisema taasisi hiyo inafanya kazi zake Tanzania bara, Ofisi Kuu ipo jijini Dodoma.

Alisema wameanza kufanya kazi halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwenye kata nne ambazo ni Ving’hawe, Mazae, Ipera na Chunyu.

Wanafanya kazi kuhakikisha vijana wanakuwa na hatma yenye mwangaza kwa kukuza uelewa wao kuhusiana na elimu ya afya ya uzazi na haki.

Pia kuandaa programu za kuzuia na kudhibiti visababishi vinavyofanya wasichana kupata mimba, kujenga uelewa wa wazazi na jamii juu ya umuhimu wa kuzungumza na watoto wa kike na kuwapa uhuru wa kueleza changamoto zinazowapelekea kupata mimba.

Akizindua taasisi hiyo kwa niaba ya Mkuu ya Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi, Kiongozi Mstaafu wa Mkoa wa Dodoma wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS), Profesa Manoris Meshack aliitaka taasisi hiyo kufanya kazi kwa misingi ya uwazi na wajibikaji ili kuunganisha nguvu na kupata matokeo makubwa.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi