loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waganga tiba asilia kuwa na hospitali

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera amesema wanajenga hospitali ya kisasa ya waganga wa tiba asilia ili watoke vichochoroni.

Amesema, hospitali hiyo inajengwa Kambungu wilayani Tanganyika, na kwamba, hiyo ni fursa pia kwa waganga wengi waliopo katika wilaya hiyo na maeneo mengine mkoani humo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kata ya Tongwe kwenye wilaya ya Tanganyika ina waganga 1,500 wa tiba asilia.

Amesema waganga wa tiba asilia Katavi wanachangia kuijenga hospitali hiyo na halmashauri inawasaidia kuwaandalia michoro.

"Wagonjwa wa kisukari watakuwa na chumba chao, magonjwa ya moyo, lakini tutakuwa tunatibu kwa awamu, mwezi huu wanakuja watu kutoka Halmashauri ya Mpimbwe, watatibu, mwezi ujao wanakuja wa Halmashauri ya Tanganyika" amesema Homera.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi