loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa ataka tathmini migogoro misikitini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameaigiza viongozi wa dini wajitathimini kwa nini kuna migogoro ya kugombea uongozi kwenye misikiti na taasisi za dini.

Ametoa agizo hilo kwenye viwanja vya Benki Tanzania (BOT) jijini Mwanza wakati wa Baraza la Maulid Kitaifa kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).

“Tutafute majawabu ya maswali haya kwa ajili ya waumini wetu ambao tunawaongoza wakati wote…unaweza kuteuliwa kuwa Shehe au Imamu lakini huwezi kuwa kiongozi bora mpaka pale uteuzi au kuchaguliwa kwako kutakapothibiti katika mioyo ya wale unaowaongoza”amesema Majaliwa wakati akimwakilisha Rais John Magufuli kwenye sherehe hizo.

Amesema Mtume Muhammad alikuwa kiongozi makini, hodari hivyo viongozi wa sasa wajiulize ni kwa kiasi gani wanamuenzi, na ni kwa kiwango gani uongozi wao unaacha athari njema kwenye nyoyo na fikra za waumini.

“Ni ukweli usiopingika kwamba hatuwezi kuepuka migogoro misikitini na kwenye taasisi zetu iwapo hatutajitathimini kupitia uongozi wetu” amesema na kuhimiza viongozi wa dini waziishi tabia za Mtume Muhammad.

Amempongeza Shehe Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir kwa uongozi mahiri uliowezesha kuwaunganisha Waislamu na taasisi za Kiislamu hivyo kupunguza migogoro kwa kiwango kikubwa.

“Na sasa nina imani kubwa utaendelea kuunganisha nguvu ndani ya nchi na kwenye mataifa jirani kama ambavyo nimeona umekaribisha mataifa jirani kwenye shughuli hii ya maulid”amesema Waziri Mkuu na kusisitiza uwepo wa mshikamano wa kidini ili kuisaidia Serikali kuleta amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Amewaomba Waislamu kuendelea kumuombea Rais John Magufuli, viongozi wengine, kuwashauri na kutoa maoni yao kuhusu mustakabali wa Taifa.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi