loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Fifa yamshushia rungu Malinzi

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), limemfungia Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi miaka 10 kujishughulisha na soka baada ya kumtia hatiani kwa matumizi mabaya ya fedha.

Mbali na kifungo hicho, Fifa imempiga faini ya dola za Marekani 503,000 (zaidi ya Sh bilioni moja). Fifa ilitoa uamuzi huo kupitia kamati yake ya Maadili baada ya kumkuta Malinzi na hatia ya matimizi mabaya ya fedha akiwa kiongozi wa TFF.

Taarifa hiyo ilisema, adhabu ya Malinzi imeanza kutumika Novemba 8 mwaka huu. Fifa imedai kwamba Malinzi alipokea Dola za Marekani 528 000 kulipa mikopo aliyodai Shirikisho linadaiwa, lakini alishindwa kubainisha matumizi sahihi ya fedha hizo.

Pia Malinzi alipokea fedha nyingine Dola za Marekani 55,000 zilizokuwa zawadi kwa ajili ya timu ya Taifa ya Soka ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo, Gabon 2017 ambazo pia matumizi yake hayakuainishwa.

Fifa imebainisha kwamba Malinzi aliyekuwa mjumbe wa kamati ya maendeleo alikuwa akitoa fedha kwenye miradi yote ya duniani wakati alipokuwa kwenye jukumu hilo kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 ndipo alipochukua fedha hizo kinyume na taratibu.

Wakati hayo yakiendelea Fifa, Malinzi ana kesi mahamakani akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha ikiwemo kutakatisha fedha na Novemba 20 mwaka huu ndio inatarajiwa kutolewa hukumu. Katika kesi hiyo Malinzi anashitakiwa na aliyekuwa katibu wake Selestine Mwesigwa, aliyekuwa karani wa ofisi Flora Rauya na aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: ZURICH, Uswisi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi