loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtanzania alipwa zaidi kwenye kikapu Rwanda

KOCHA Mtanzania anayefundisha mpira wa kikapu nchini Rwanda, Henry Mwinuka ambaye sasa amejiunga na timu ya Rwanda Energy Group (REG) ndiye anayelipwa mshahara mnono zaidi nchini humo, imeelezwa.

Mwinuka hivi karibuni alijiunga na REG baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha timu ya kikapu ya Patriots, anaweka kibindoni Dola za Marekani 3,000 (sawa na Sh 6,912,000) kila mwezi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, Mwinuka ambaye kwa sasa ndiye Kocha Mkuu wa REG, alimaliza kibarua chake cha kuifundisha Patriots kwa miaka minne kuanzia 2015 na kuipatia mafanikio makubwa timu hiyo katika kipindi chake.

Kwa sasa Patriots wanafundishwa na Mkenya, Fracis Odhiambo ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kenya, ambaye akichukua nafasi ya Mwinuka na juzi alifanikiwa kuifunga REG katika fainali.

Patriots walifanikiwa kushinda robo ya mwisho ya mchezo huo kwa 68-59 baada ya kuizidi REG katika robo tatu za mwanza. Akizungumza katika mahojiano maalumu na Times Sport, Odhiambo alisema amefurahi sana kupata nafasi ya kuifundisha timu kubwa kama hiyo ya mpira wa kikapu nchini Rwanda, na sasa anaangalia mbele kupata mafanikio zaidi.

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi