loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stars yatamba kupata dawa ya Equatorial Guinea

WAKATI joto la mchezo wa kusaka nafasi ya kushiriki fainali ya mataifa Afrika Afcon 2021 Cameroon likizidi kupanda kati ya timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars na Equatorial Guinea kocha msaidizi wa timu hiyo, Selemani Matola ameanika mikakati ya kuwafunga wapinzani wao.

Stars inatarajiwa kucheza na Equatorial Guinea Ijumaa ya wiki kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kabla ya kucheza na Libya siku nne baada ya hapo. Akizungumza Dar es Salaam jana, Matola alisema kucheza mchezo wa kushambulia muda wote kusaka mabao mengi ndiyo mbinu wanazowapa wachezaji wa kikosi hicho katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa kuhakikisha wapinzani wao hawachomoki.

“Kambi yetu ni ya muda mfupi hivyo kilichabaki tunawapa wachezaji mbinu ya kupata ushindi dhidi ya Guinea… tutaingia kwa stahili ya kushambulia muda wote kutafuta ushindi na huku tukizuia tusifungwe,” alisema Matola.

Alisema kupitia mbinu hiyo kushambulia muda wote na kujilinda wanaamini watapata matokeo baada ya kuangalia mikanda ya video za wapinzani wao hao kwenye michezo yao iliyopita. Alisema kulingana na ratiba ngumu waliyonayo baada ya mchezo huo Ijumaa, alfajiri ya Jumamosi kikosi hicho kinatarajia kuanza Safari ya kuelekea Tunisia itakapochezwa mechi hiyo.

Stars ipo kundi J pamoja na Libya, Equatorial Guinea na Tunisia, timu mbili za juu zitasonga mbele. Timu nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zitakazokuwa viwanjani wiki hii kwa ajili ya michuano hiyo ni Rwanda itakayokuwa ugenini kucheza na Msumbiji keshokutwa na Kenya itakuwa ugenini dhidi ya Misri. Kesha Uganda itakuwa ugenini dhidi ya Bukinafaso.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi