loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa ataka Waislamu waendelee kusaidia jamii

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kusaidiana katika masuala ya kimaendeleo, ikiwemo elimu ya juu. Aidha, amewapongeza kwa kushiriki kuiendeleza jamii ya Kitanzania.

Majaliwa alitoa mwito huo juzi wakati akizungumza kwenye Baraza la Maulid lililofanyika mkoani Mwanza ambapo alibainisha kuwa dini ya Kiislamu ni chachu ya maendeleo kwa kuwa elimu ndio msingi wa maendeleo hayo na ana imani kuwa kwa kupata elimu bora zaidi vijana wa kiislamu watashiriki kikamilifu katika maendeleo.

Alisema kwa upande wa serikali, fedha nyingi zimetengwa kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bure kuanzia ya msingi hadi sekondari huku ile ya vyuo vikuu ambayo inapaswa kulipiwa kubaki kuwa ni jukumu la jamii pia kuchangia.

“Serikali imetenga zaidi ya Sh bilioni 450 kuwakopesha wanafunzi kupata elimu ya juu, hivyo ni wazi kuwa kiasi hicho cha fedha si kwamba kitawatosha wote ila kwa wale ambao labda hawatapata kiwango chote ni jukumu letu kusaidiana hasa katika ngazi za kifamilia,” alisema.

Alisema kuwa kaulimbiu ya Bakwata ya Jitambue, Badilika na Acha Mazoea, inatoa mwanga mzuri zaidi wa utendaji kazi wa Waislamu hasa katika kujiendeleza kwenye nyanja tofauti za uchumi, kijamii huku akisisitizia nafasi ya dini hiyo katika kutunza na kuendeleza amani ya nchi.

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi