loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hakuna fidia askari waliostaafu bila vyeo

SERIKALI imesema haina utaratibu wa kulipa fi dia kwa askari ambao hawakupandishwa vyeo mpaka wanastaafu. Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Yusuf Masauni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Juma (CCM). Katika swali lake, Juma alitaka kujua kama serikali ina mpango wa kuwalipa fidia askari ambao wamekosa haki zao kwa kutopandishwa vyeo kwa wakati mpaka wanastaafu.

Masauni alisema, suala la fidia ya aina hiyo halipo na kuwa upandishwaji wa vyeo kwa askari unafanywa kwa utaratibu na kwa siku za hivi karibuni tayari wameshapandisha vyeo askari wapatao 9,000 wa jeshi la polisi pekee.

Katika swali la msingi, Juma alitaka kujua serikali ina mfumo gani wa kupandisha madaraja askari wenye vyeo vya chini. Akijibu swali hilo, Masauni alisema vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani vina mfumo wa upandishwaji wa madaraja kwa askari wa vyeo vya chini ambavyo huzingatia vigezo mbalimbali.

Alitaja baadhi ya vigezo kuwa ni miaka mitatu ya cheo alichonacho, tabia njema, nidhamu, utendaji mzuri, umahiri wa kazi na elimu.

“Vigezo vingine ni utaalamu mahsusi, uwezo wa kumudu madaraka ya cheo anachopandishwa, kutokuwa na tuhuma zinazochunguzwa wala mashtaka ya kijeshi katika kipindi cha miaka mitatu na bajeti tengefu kwa mwaka husika,” alisema.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi