loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake washauriwa kuthubutu, kujiamini

WANAWAKE wametakiwa kujenga tabia ya uthubutu, kujiamini ili kufi kia mafanikio makubwa kwenye biashara wanazozifanya na kuachana na kasumba kuwa elimu ndio kigezo cha kufi kia mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki mjini hapa na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri wakati wa kongamano la wajasiriamali. Alisema mwanamke ni chachu ya maendeleo kiuchumi, ndio wenye viwanda na wanaokuza uchumi wa nchi.

“Tujiulize kwa nini hatumiliki biashara kubwa, kila unapoamka unatakiwa uwaze jambo fulani, kila siku fanya maamuzi ya kujitathimini na uwe na uhuru wa masuala ya fedha,” alisema.

Maida ambaye pia ni Mkurugenzi wa IBRA Contractors, alisema lazima kutengeneza afya ya fedha kwani unapofanya biashara kisha hupati fedha huo ni kama utapiamlo.

“Angalia changamoto kama fursa, elimu si kigezo cha kufikia fursa, mimi nilipata tuzo ya mkandarasi bora nikiwa na elimu ya kidato cha nne tu lakini niliajiri wataalamu, baadaye nikajiendeleza na sasa nina diploma ya juu na bado ninaendelea kusoma,” alisema.

Alisema amekuwa mmiliki wa kampuni tano zinazofanya vizuri katika biashara kwa vile hakuona elimu kama kigezo cha kushindwa kufikia malengo yake.

“Wanawake wengi ukiwauliza kwa nini hujafanya vizuri anasema kwa sababu hajasoma,” alisema.

Alisema kigezo cha elimu kimekuwa kikiwafanya wanawake wengi kurudi nyuma kwenye biashara.

“Mimi wakati naanza sikuwa na mtaji mkononi ila kisaikolojia nilikuwa nasema mimi ni tajiri, lazima ujue unataka nini, uko wapi na unakwenda wapi kwa maana unapoingia kwenye mapambano lazima ujue thamani yako,” alisema.

Pia alisema tabia inaweza kuwa kikwazo kwa baadhi ya watu lakini lazima kufanya kazi kwa bidii. “Vitu vinavyotakiwa ili vikutoe mahali ulipo ni msukumo, ujuzi au kipaji, kujiamini na nidhamu.

Alisema kama huna nidhamu huwezi kufanikiwa unatakiwa kutafuta fedha kwanza ndio utafute biashara, pia kuwa mbunifu kwani maisha hayajawahi kuwa rahisi na changamoto ziko kila siku na kusimamia unachokiamini. Kwa upande wake, mwezeshaji katika kongamano hilo ambaye ni mshauri wa biashara, Joan Manda alisema wanawake wana nguvu kubwa ndani yao.

Alisema kuna mstari mwembamba sana ambao hauonekani kati ya wajasiriamali na wafanyabiashara, tofauti ni kuwa mfanyabiashara anathubutu na ana maamuzi.

“Ukikakaa unang’ang’ania ujasiriamali huwezi kuwa mwekezaji, katika hili wanawake wanaweza sana ni maamuzi ya kuamua kubadilika,” alisema.

Alisema kwenye mafanikio kila mmoja anatakiwa kuwa na maana yake na ukipima kupitia kwa mtu mwingine huwezi fanikiwa.

“Usipokuwa na mipango huwezi kufanikiwa, jiruhusu kuwa mwanafunzi kila siku,” alisema.

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi