loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Idadi ya Wakenya yafikia milioni 47.5

MATOKEO ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Agosti, mwaka huu nchini Kenya, yameonesha idadi ya watu nchini humo imeongezeka na kufi kia 47,564,296.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Takwimu nchini Kenya, sensa hiyo hufanyika kila baada ya miaka 10 na kwa matokeo hayo kuna ongezeko la watu milioni tisa kwa kipindi hicho.

Takwimu zinaonesha kuwa, kati ya idadi hiyo ya watu, kuna wanawake milioni 24 na wanaume milioni 23.6, huku watu wenye jinsia tata wakiwa 1,524. Wiki iliyopita Rais Uhuru Kenyatta alipokea ripoti ya sensa hiyo na kusema Kenya imekuwa nchi ya kwanza duniani kupata matokeo ya idadi ya watu kwa kipindi kifupi cha miezi miwili.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kaunti ya Nairobi inaongoza kwa wingi wa watu ambao wamekadiriwa kuwa zaidi ya milioni 4, ikifuatwa na Kiambu, Nakuru, Kakamega na Kilifi.

Sensa hiyo ni ya kwanza baada ya nchi hiyo kupata katiba mpya mwaka 2010 na inatarajiwa kuisaidia serikali kuweka mipango ya maendeleo na kugawa rasilimali mbalimbali kwa ajili ya NAIROBI maendeleo ya raia wake.

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi