loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tshisekedi, Museveni waahidi kukuza biashara

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi (pichani) yuko Uganda kwa lengo la kukuza biashara baina ya mataifa hayo mawili jirani, hatua ambayo inatarajiwa kuwa chachu ya uhusiano mzuri wa kibiashara na kidiplomasia kati ya nchi hizo.

Baada ya kukutana na kiongozi huyo wa DRC, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema mataifa hayo mawili yatajenga ushirikiano madhubuti utakaoimarisha biashara, uwekezaji na utalii kwa pande zote mbili.

Alisema nchi hizo zitajenga barabara na madaraja yatakayounganisha mataifa hayo mawili na kwamba hatua hiyo ina shabaha za kibiashara, ustawi wa jamii na ulinzi. Biashara kati ya mataifa hayo mawili kwa mwaka uliopita ilifikia thamani ya Dola za Marekani milioni 513, lakini kwa sasa kuna ishara ya kuongezeka baada ya Uganda kuelekeza nguvu zake nchini DRC.

Museveni na Tshisekedi wamekubaliana kujenga barabara ya umbali wa kilometa 1,200 kuanzia Uganda kuelekea katika miji mitatu ya eneo la Mashariki mwa Kongo ya Goma, Bunia na Beni.

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi