loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Soko la kahawa Uganda sasa laimarika Urusi

KAHAWA ya Uganda imepata bahati ya kupigiwa chapuo katika soko kubwa lenye watumiaji wengi wa kahawa nchini Urusi.

Baada ya kufanya vizuri katika masoko ya nchi za Ulaya Magharibi kwa muda mrefu, Uganda imeanza kutangaza kahawa yake katika nchi za Ulaya Mashariki na sasa iko katika soko kubwa duniani la kahawa nchini Urusi.

Kwa mujibu wa taasisi ya uzalishaji wa kahawa nchini Urusi (Rusteacoffee), soko la kahawa nchini humo lina thamani ya Dola za Marekani milioni 750. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo kubwa ya kahawa katika nchi hiyo, thamani ya soko la kahawa kwa sasa imepanda hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.5. Takwimu hizo zimeonesha kuwa, kila mwananchi wa Urusi anaweza kutumia kahawa kilo 1.7.

Kiwango hicho ni kikubwa ikilinganishwa na idadi ya wananchi wa nchi hiyo. Kwa hali hiyo, ina maana kila mwananchi wa nchi hiyo anakunywa vikombe vya kahawa 120 kwa mwaka.

Hii inaonesha Urusi ni soko kubwa na muhimu kwa biashara ya kahawa ya Uganda. Katika kuhakikisha kuwa kahawa ya Uganda inatangazwa vya kutosha katika soko la kahawa nchini Urusi, Mamlaka ya Ustawishaji wa Kahawa Uganda (UCDA) imeungana na ubalozi wa nchi hiyo mjini Moscow katika maonesho ya aina mbalimbali za kahawa na chai yaliyofanyika katikati ya mwezi uliopita.

Uganda ni moja ya mataifa ya Afrika Mashariki yanayozalisha kahawa kwa wingi na imefanikiwa kuwa na kahawa yenye ubora wa hali ya juu. Ubora huo umechangia kwa kiasi kikubwa kukubalika kimataifa na kujipatia masoko katika mataifa mengi duniani. Mataifa mengine ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayozalisha kahawa kwa wingi ni Tanzania, Kenya na Rwanda.

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi