loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiir, Machar wapewa siku 100 serikali umoja kitaifa

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir na Kiongozi wa Waasi, Riek Machar, wamepewa siku nyingine 100 ili waunde serikali ya pamoja baada ya kushindwa kumaliza tofauti zao kwa muda mrefu.

Maamuzi hayo yalifikiwa jijini Kampala, Uganda wakati viongozi hao walipokutana na Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, kipindi kilichopangwa kitamalizika Novemba 12, mwaka huu lakini sasa kimeongezwa miezi mitatu.

Tume ya upatanishi inatarajia kuwa tarehe hiyo ni ya mwisho na itazuia Sudan Kusini kutumbukia tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Serikali ya mpito ilikuwa na jukumu la kuzikutanisha pamoja pande hizo mbili hasimu na kumaliza tofauti zao, lakini, kutokana na kuahirishwa mara ya kwanza na ya pili, sasa serikali hiyo inatarajiwa kutangazwa Februari, mwakani.

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi