loader
Picha

Magufuli- Nilinyweshwa sumu Dodoma

Rais John Magufuli amesema hawezi kusahau namna sifa alizopewa na Rais Benjamin Mkapa kumuita askari wake wa mwamvuli namba moja zilivyomsababishia matatizo likiwemo la kunyweshwa sumu Dodoma.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Rais Mkapa alimsifu kwa kuwa alifanya kazi nzuri kwenye ujenzi wa barabara na amemshukuru kiongozi huyo kwa kumuamini.

"Nilianza kuona dalili za baadhi ya mawaziri tena wengine wa ngazi za juu kabisa kuanza kunichukia na muda si mrefu baada ya hapo ninyweshwa sumu Dodoma ambayo almanusura iondoe uhai wangu lakini kwa neema za Mwenyezi Mungu nikakiepuka kifo"- amesema Rais Magufuli na kubainisha kuwa aliamua kujiuzulu.

"Baada ya tukio la kunusurika kifo nilimwendea mzee Mkapa kumweleza dhamira yangu ya kutaka kujiuzulu. Nakumbuka siku hiyo aliniangalia kwa jicho la baba na mwana akinihurumia lakini pia kunipa ujasiri na baada ya dakika chacha akaniambia 'John kafanye kazi, kamtangulize Mungu, baada ya hapo nikapewa ulinzi nikaendelea kuchapa kazi"amesema.

Amesema wakati akiwa na Rais Mkapa kwenye tukio hilo alimwona kiongozi huyo kuwa ni mtu anayekupa matumaini hata kama umekata tamaa.

“Mzee Mkapa nakushukuru sana, nimejifunza kutokuwasifu wateule wangu hata kama wanafanya mazuri mengi kwa sababu ninajua yasije yakawapata yaliyonipata mimi baada ya wewe kunisifu. Lakini hata hivyo wakati mwingine ninashindwa huwa ninawasifu baadaye nakwenda kukumbuka hayo yaliyonipata”amesema.

Amesema hawezi kumsahau mzee Mkapa kwa yaliyotokea wakati wa harakati za uchaguzi mwaka 2015 alipokwenda kwa marais wastaaf akiwemo mzee Mkapa kuwaeleza nia yake kugombea urais wa Tanzania.

“Kwanza kabisa wakati mimi nataka kwenda kwa mzee Mkapa nikagundua wagombea wenzangu wote wa CCM walikuwa tayari wameshaenda. Hapa ikanikumbusha historia kwenye Biblia ya Isaka na Yakobo, hata hivyo sikukata tamaa nami nikaenda na kumweleza mzee Mkapa kuhusu dhamira yangu ya kutaka kuwania urais. Kwa dakika kadhaa mzee Mkapa hakunijibu kitu..."amesema na kubainisha kuwa baada ya muda mzee Mkapa alimweleza ‘John kamtangulize Mungu’.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi