loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rage atia neno hukumu ya Malinzi Fifa

MAKAMU wa rais wa zamani wa Shirikisho la soka Tanzania, TFF, Ismail Rage (pichani) amewataka viongozi wa soka kujifunza kutokana na kifungo cha Jamal Malinzi Fifa.

Juzi, Shirikisho la soka la kimataifa, Fifa lilimfungia rais wa zamani wa TFF Malinzi miaka 10 kujihusisha na soka na kumtoza faini ya zaidi ya Sh bilioni moja kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Malinzi anakuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu za soka kutoka Tanzania kukumbwa na adhabu ya aina hiyo ya Fifa. Rage ambaye pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa kilichokuwa Chama cha soka nchini, Fat, sasa TFF alidai kifungo hicho ni fundisho kwa watu wote wanaopenda madaraka wakiwa na dhamira ya kujinufahisha wao na maisha yao ikiwa ni tofauti na matakwa na miongozi ya taasisi kubwa zinazotegemewa na jamii.

Akizungumza jana na gazeti hili kwa njia ya Simu Rage aliyewahi pia kuwa mwenyekiti wa Simba alisema wapena soka wanatakiwa kufahamu kuwa rais wa sasa wa Fifa, Gianni Infantino hana masikhara kwenye uongozi wake na kwamba anataka uchapaji kazi.

Alisema jambo hilo liwaingia mashabiki na wanachama wa klabu za Simba na Yanga na kwamba wabadilike kuwabana viongozi wao kwenye matumizi ya fedha badala ya kutaka ushindi pekee.

“Kufungiwa kwa Malinzi hakuna mtu anayeweza kukataa, bali linapaswa kuwa funzo kwa watu wote ambao wanakimbilia madaraka kwa lengo la kujinufaisha wenyewe binafsi na maisha yake tofauti na matakwa ya taasisi na wajue kipindi cha rais Infantino hana masikhara kabisa,” alisema Rage.

Rage alisema endapo wanachama na Simba na Yanga watapata elimu kuhusu suala la ukaguzi wa hesabu kwa viongozi wao, wataokoa fedha nyingi ambazo viongozi wao wanatumia bila kuweka vizuri mchanganuo wa matumizi yake.

Mbali na adhabu hiyo, Malinzi ambaye kwa sasa yupo mahabusu, anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya na utakatishaji fedha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na inatarajiwa kutolewa hukumu Novemba 20.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi