loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kilimanjaro Queens akili yote kwa Sudan

KOCHA mkuu wa timu ya Soka ya taifa ya wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens ,Bakari Shime amesema morali ya kikosi hicho ipo juu tayari kwa kuwakabili Sudan Kusini kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi A katika michuano ya kombe la Chalenji.

Michuano hiyo inayofanyika chini ya usimamizi wa Baraza la vyama vya soka Afrika Madhariki na Kati, Cecafa inatarajiwa kuanza Jumamosi ya wiki hii kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi ikishirikisha timu nane. Queens ambao ni mabingwa watetezi mara mbili mfululizo watakuwa na kibarua hicho mbele ya Sudan siku ya ufunguzi wa michuano hiyo na tayari kikosi hicho kipo kwenye maandalizi kabambe.

Akizungumza jana Dar es Salaam Shime alisema morali ya kikosi ipo juu pamoja na kwamba mazoezi mepesi yanaendelea kutolewa kwa kikosi hicho.

“Morali ya kikosi cha Queens ipo juu na kwa sasa kwa vile muda bado benchi la ufundi tunaendelea kuwapa mazoezi mepesi kuweka sawa miili yao tayari kwa mchezo wetu ambao tunahitaji zaidi ushindi kubusti malengo yetu,” alisema Shime .

Alisema mazoezi anayoendelea kuwapa vijana hao ni namna ya kutoa pasi imfikie mlengwa kwa wakati pamoja na kuwaelekeza nidhamu kwa muda wote wakiwa uwanjani. Shime alisema pamoja na kwamba mechi hiyo itakuwa na upinzani bado anaamini ubora wa mchezaji mmoja mmoja unaweza kuwapa majibu sahihii hususan kwenye kuamua matokeo uwanjani.

Timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo ni Tanzania Bara, Zanzibar,Burundi na Sudan zilizo kundi A na kundi B likiwa na timu za Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibouti.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi