loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasanii kutoa tuzo kwa Nyerere

MASHIRIKISHO ya sanaa nchini yanatarajia kutoa tuzo ya heshima kwa viongozi mbalimbali akiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia hiyo.

Pia yamepanga kumpa tuzo Rais John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein kutokana na michango yao ya kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere katika uongozi wao.

Tuzo hizo zinatarajiwa kukabidhiwa keshokutwa katika tamasha lililoandaliwa na mashirikisho hayo manne ya sanaa za maonesho, ufundi, muziki na filamu. Katika tamasha hilo, litakaloanza kwa kongamano la wasanii, Rais Magufuli atafungua pamoja na kukutana na wasanii.

Hayo yalisemwa jana nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Mikocheni Dar es Salaam baada ya viongozi wa shirikisho hizo kwenda kushukuru familia ya Mwalimu kutokana na mchango aliouonesha wakati wa uhai wake.

Akizungumza jana, Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifamba alisema lengo la tamasha hilo lililoandaliwa na wasanii ni kutambua mchango wa mwalimu lakini pia kutangaza aliyoyafanya ili wale walio na umri wa miaka 20 kwa sasa ambao hawakumfahamu wamfahamu.

“Hatutaki historia ife, wapo wasiomjua mwalimu na ni wale ambao wenye miaka 20 kwa sasa, hivyo tutatumia sikuhiyo kumzunguzia mwalimu kama kiongozi mashuhuri kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Mwakifamba.

Alisema katika tamasha hilo litaambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo burudani, mashairi, nyimbo na hata video ili kizazi cha sasa kiendelee kumtambua mwalimu kwa kazi mbalimbali alizofanya.

Akiwapokea wasanii nyumbani kwa Mwalimu Mikocheni, mtoto wa Mwalimu, Makongoro Nyerere alitumia muda mwingi kueleza ratiba ya mwalimu wakati wa uhai wake kuanzia asubuhi hadi jioni na kuwashukuru kwa kukumbuka mchango uliotolewa na Mwalimu.

Alisema Mwalimu Nyerere pamoja na waasisi wenzake waliwatumia wasanii katika harakati mbalimbali, na kuwapongeza kwa kutambua suala hilo. Makongoro aliyekuwa akiwafurahisha wasanii kwa muda mrefu kutokana na maelezo yake, alisema kwa sasa amerudi CCM na ni mjumbe wa Halmashauri Kuu.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi