loader
Picha

Mkude aondolewa Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Etienne Ndayiragije amemruhusu kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude kurudi nyumbani ili kushughulikia matatizo yake ya kifamilia.

Siku chache zilizopita kiungo huyo wa Simba alitoa taarifa kwa kocha wake kuwa anahitaji muda wa kuwa karibu na familia yake na kutatua baadhi ya mambo, lakini muda aliopewa haukutosha hivyo juzi aliomba ruhusu nyingine na kuruhusiwa jana.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Shirikisho la soka Tanzania, TFF ilisema kuwa kutokana na muda mchache uliobakia kabla ya kucheza mchezo wa kuzufu fainali za kombe ya mataifa Afrika, Afcon 2021 dhidi ya Equatorial Guinea keshokutwa, kocha huyo hatochagua mchezaji mwingine wa kuziba nafasi ya kiungo huyo.

Kiungo huyo atalazimika kusubiri mchezo wa pili dhidi ya Libya utakaochezwa wiki iyajo endapo masuala yake yatakuwa sawa. Taifa Stars inaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kujiweka sawa kabla ya mechi hiyo.

MABONDIA Watanzania wametakiwa kujiaandaa vyema kabla ya kwenda kushiriki kwenye ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

2 Comments

 • avatar
  KULWA PAULO
  13/11/2019

  Comment

 • avatar
  moxhi
  14/11/2019

  Comment

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi