loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbunge ataka uzazi wa mpango kwa wanaume

MBUNGE Viti maalum, Khadija Nassir (CCM), ameitaka serikali kuanzisha programu za uzazi wa mpango kwa wanaume, akisema tafi ti zimeonesha mwanaume mmoja ana uwezo wa kuwapa mimba wanawake tisa kwa siku moja.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Nassir alisema tafiti mbalimbali duniani zimeonesha mwanaume mmoja ana uwezo wa kuwapa mimba wanawake tisa kwa siku moja, wakati mwanamke mmoja ana uwezo wa kushika mimba moja kwa miezi tisa.

“ Je, serikali haioni kuendelea na programu za uzazi wa mpango kwa wanawake ni uharibifu wa rasilimali, badala yake programu za uzazi wa mpango zifanyike kwa akina baba?,” alihoji.

Akijibu, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile, alisema ni dhana potofu kudhani kwamba uzazi wa mpango ni kwa ajili ya wanawake peke yao.

“Suala la uzazi wa mpango linawahusu wanaume vile vile na sisi kama serikali tunahamasisha akina baba na mama wanashiriki kwenye uzazi wa mpango salama,” alisema.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Zubeda Sakuru, alihoji serikali ina mkakati gani wa kuwawezesha wakunga wa jadi ili kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua hasa maeneo ya vijijini.

Akijibu, Dk Ndugulile alisema Tanzania iliridhia mkataba wa uzazi salama mwaka 1994 katika mkutano uliofanyika nchini Misri.

“Mkataba huo unaelekeza kwamba, kila mama anayejifungua atahudumiwa na mtaalamu mwenye ujuzi, kwa kutilia maanani kwamba, matatizo yatokanayo na uzazi hayatabiriki na yakitokea huhitaji kutatuliwa na wataalamu wenye ujuzi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto mchanga,” alisema.

Dk Ndugulile alisema wizara hiyo inatambua wakunga wa jadi ni watu muhimu katika jamii, hivyo inawatumia kufanya uhamasishaji wa wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma na ikibidi kuwasindikiza.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi