loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC awapa somo watumiaji bandari ya Kigoma

WATUMIAJI wa Bandari ya Kigoma na mpaka wa Manyovu mkoani hapa, wametakiwa kutambua kuwa wao ni sehemu muhimu katika kuendeleza sekta binafsi, inayochangia uingizaji wa mapato, ajira na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga wakati wa ufunguzi wa semina ya wazalishaji, wasindikaji wa bidhaa na watumiaji wa Bandari ya Kigoma na mpaka wa Manyovu.

Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Katibu Tawala anayeshughulikia uchumi na uzalishaji, Dk Vedast Makota alisema elimu itakayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) itawawezesha washiriki kujua taratibu za kufuatwa wakati wa uingizaji na uthibitishaji wa bidhaa na changamoto zinazohusu mifumo na taratibu husika.

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa TBS, Gervas Kaisi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Athuman Ngenya, alisema ili kwenda sanjari na mikakati ya kitaifa, TBS imeendelea kutoa semina kwa wazalishaji na waagizaji wa bidhaa mbalimbali zitokazo nje katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Tanga na Kilimanjaro.

Alisema kwa kuzingatia Kifungu cha 36 cha Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009, serikali ilipitisha Kanuni za Udhibiti wa Shehena kupitia Notisi ya Serikali Namba 405 ya Desemba 25, 2009.

Kaisi alisema kanuni hizo, ziliipa TBS mamlaka ya kudhibiti ubora wa bidhaa, zinazoingia nchini kabla ya usambazwaji kwenye soko la ndani. Hivyo, waagizaji wa bidhaa wanapaswa kufanya biashara bila kukinzana na kanuni zilizopo.

Alisema mbali na kanuni hizo, Februari mosi mwaka 2012 TBS ilianzisha mfumo wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya usafirishwaji kuja nchini, kama mpango wa udhibiti ubora wa bidhaa katika nchi zinakotoka. Mpango huo unasaidia kutatua changamoto zilizokuwepo wakati bidhaa zilipokuwa zinakaguliwa baada ya kufika nchini.

Alitaja changamoto hizo ni ucheleweshaji wa kuondosha mizigo bandarini, kuwepo kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje wasio waaminifu wanaopitia njia za panya na kukosekana kwa vifaa vya kisasa vya kupimia kila bidhaa inayoingizwa hapa nchini. Mpango wa udhibiti ubora wa bidhaa unaongozwa na kanuni ya uingizaji wa bidhaa nchini, upo kwa mujibu wa Kifungu cha 4 (1) (s) cha Sheria ya Viwango Namba 2 ya 2009.

TBS ilikasimu kazi ya ukaguzi wa bidhaa huko zinakotoka kwa kampuni za kimataifa, zinazofanya ukaguzi maeneo mbalimbali duniani kote. Kampuni hizo ni SGS, Bureau Veritas, Intertek na CCIC ambazo hukagua shehena hizo kwa niaba ya TBS na kutoa cheti cha ubora, baada ya kujiridhisha kuwa bidhaa husika zinakidhi matakwa ya viwango husika.

Pia kuna mfumo wa kukagua shehena za bidhaa baada ya kuwasili nchini, kabla ya kuruhusiwa kuingia kwenye soko. Ukaguzi huo hufanyika mipakani, bandarini na viwanja vya ndege.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi