loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polepole- Uchaguzi si kombolela

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu ni mchakato muhimu kuwapatia wananchi viongozi na si kama mchezo wa kombolela.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa CCM itashiriki uchaguzi huo na itafanya kampeni za kistaarabu.

Amesema, CCM itakuwa na wagombea 333,000 na kutakuwa na watu 1, 379,000 watakaosimamia uchaguzi huo.

“Mtu yeyote mwenye akili timamu ataelewa kwa nini wenzetu wamekimbia mapema”amesema Polepole.

Amesema, chama hicho kina mashina zaidi ya 231,000 na kwenye kila shina kutakuwa na watu watano wa kusimamia uchaguzi huo.

“Hawa watu watano watakuwa na dhamana ya kusimamia uchaguzi katika ngazi ya shina, watu mahodari, watu mahiri, wamepikwa na tumekuwa na programu ya mafunzo kwa watu hawa watano katika ngazi ya shina. Watu hawa nchi nzima jumla yao ni 1, 039, 190, wamefunzwa kushiriki kwenye uchaguzi, kujenga hoja na kuhakikisha haki ya Watanzania inapatikana”amesema Polepole.

Amesema takribani watu 240,000 watasimamia uchaguzi kwenye zaidi ya matawi 23,000 ya CCM.

Kwa mujibu wa Polepole kuna watu 2,000 nchi nzima watakaosimamia uchaguzi kwenye ngazi ya wilaya na kitaifa kutakuwa na watu 24 wazito kwenye nchi hii.

“Katika ngazi ya kata tuna watu pale 39,000 katika zile kata 4,000. Sasa hapo ndio nitakuonyesha siri ya ushindi. Yaani katika kata zote 4,000 sisi Chama Cha Mapinduzi tumeweka watu 39,000 kwa kila kata inasimamia uchaguzi kwa hiyo utagundua tuna watu wengi kuliko kata zenyewe ambao watasimamia uchaguzi”amesema Polepole na kubainisha kuwa watu 324 watasimamia uchaguzi kwenye ngazi ya mkoa.

“Watu wamepokea mafunzo ya kutosha ya ndani na nje ya nchi. Kutoka mwaka 2016 tumekuwa tuna programu ya mafunzo kwa viongozi wa chama na watendaji ndani ya chama katika chuo chetu cha Ihemi kiko Iringa pale, chuo kikongwe na kikubwa kinapika watu. Tumekuwa na program ya mafunzo ya watu hawa 324 pale Tunguu Zanzibar, lakini pia tumeanza mafunzo ya awali Kibaha kenye chuo chetu kikuu, hawa wamepita hapo, wamepikwa…hawa watu ni hapana chezea”amesema.

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeanza rasmi ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi