loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stars wagombea namba

WAKATI mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yakiendelea kunoga, wapinzani wao Guinea ya Ikweta wanatarajiwa kutua nchini leo alfajiri tayari kwa pambano la kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcom 2021 nchini Cameroon.

Kambi ya Taifa Stars ilikamilika juzi baada ya kutua kwa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi, Mbwana Samatta kutoka Ubelgiji na Simon Msuva anayecheza soka Morocco, huku ushindani ukingezeka kwa wachezaji kugombea namba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema wachezaji wote wanaonesha kiwango kizuri mazoezini kila mmoja akisaka nafasi ya kuwamo katika mchezo huo wa kesho kwenye Uwanja wa Taifa. Mchezo huo wa kwanza wa Afcon 2021 dhidi ya timu hiyo ya Guinea ya Ikweta, utaanza saa 1:00 usiku na viingilio ni Sh 5,000 VIP na 3,000.

“Vijana wako katika ari ya juu, kila mmoja anaonesha kiwango ili aweze kupata namba katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo, tunaamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema.

Mchezaji huyo wa zamani wa Stars alisema jambo la muhimu ni mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kuwatia nguvu wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuanza kwa ushindi mchezo huo wa kwanza kabla ya kucheza na Libya katika mchezo wa pili. Kwa upande wake, Kocha Msaidizi Juma Mgunda, alisema maandalizi yanakwenda vizuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Alisema wachezaji waliopo kwa kipindi hiki watasaidia kutimiza lengo la kwanza la kutafuta ushindi katika mchezo huo wa kwanza wa kufuzu kabla ya kuelekea Tunisia kuwakabili Libya. Taifa Stars inasaka kwa mara ya pili mfululizo kufuzu kucheza fainali za Afcon baada ya mwaka huu kushiriki zile za Misri, lakini ilitolewa katika hatua ya makundi baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza miaka 39 iliyopita.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi