loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Cecafa mambo yazidi kuiva

ZIKIWA zimebaki siku mbili michuano ya Kombe la Chalenji (Cecafa) kwa wanawake kuanza kutimua vumbi nchini, mambo yamezidi kuiva kwa timu shiriki kutoka nje kuanza kuwasili tayari kwa michuano hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dare es Salaam, Katibu wa Chama cha Soka la Wanawake nchini, Somoe Ng’itu, alisema michuano hiyo inashirikisha timu nane zilizopangwa katika makundi mawili ya A na B na kwamba maandalizi ya mapokezi kwa timu shiriki yanaenda vizuri.

Alisema hadi sasa ukiwatoa wenyeji Kilimanjaro Queens , timu nne ambazo ni Burundi, Kenya, Djibout na Ethiopia zimeshawasili nchini tangu jana na leo zinatarajia kutua timu za Uganda, Sudan Kusini na Zanzibar.

“Maandalizi yanaenda vizuri kama tulivyopanga na hadi sasa tumeshapokea timu nne, ambazo ni Burundi, Kenya, Ethiopia na Djibout na nyingine tatu tunatarajia kuzipokea kesho (leo), ambazo ni Uganda, Sudan Kusini na Zanzibar tayari kwa michuano itakayoanza Jumamosi, “ alisema.

Ng’itu alisema maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika sambamba na viwanja vya kufanyia mazoezi kwa timu hizo, ambapo wameanda viwanja vitatu vya Azam Complex Temeke, Karume na JMK Park Kidongo Chekundu, vyote vya Ilala .

Timu hizo zimepangwa kwenye makundi mawili, ambapo Kundi A lina timu za Kilimanjaro Queens ambao ni wenyeji na mabingwa wa tetezi mara mbili mfululizo na timu za Zanzibar, Burundi na Sudan Kusini, wakati Kundi B linaundwa na timu za Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibout.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Baraza la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho hadi Novemba 27.

WACHEZAJI na viongozi wa Simba SC wamewasili jijini Dar es ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi