loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Real kuvunja benki kumsajili Mbappe

VIGOGO vya Hispania, Real Madrid, wanafi kiria kumsajili kwa rekodi ya dunia ya pauni milioni 400 nyota wa klabu ya Paris Saint Germain (PSG), Kylian Mbappe, imeelezwa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akihusishwa na kuhamia kwa vijana hao wa Los Blancos tangu wakati akiwa katika Ligi ya Ufaransa ya Ligue 1 na AS Monaco, lakini badala yake alitua kwa mahasimu wao wa ligi PSG kwa ada ya pauni milioni 135.

Hivi karibuni, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa mara ya nyingine tena alikuwa akihusishwa na kujiunga na mabingwa hao mara 13 wa Ulaya na kwa taarifa zilizopita, Real Madrid wako mbioni kumsajili na wako tayari kutoa pauni milioni 400 kwa klabu hiyo ya Ufaransa.

Ofa hiyo ni kama mara mbili katika historia ya usajili katika soka, baada ya Neymar ambaye alijiunga na PSG akitokea timu ya Hispania ya FC Barcelona kwa ada ya pauni milioni 222 katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2017.

Rekodi ya Mbappe katika umri mdogo amefunga mabao 67 na kutoa usaidizi wa magoli mara 31 katika mechi 104 za ligi.

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi