loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Salah kukosa mechi za Misri

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah, atakosa mchezo wa timu ya taifa lake la Misri wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2021, dhidi ya Kenya na Comoros kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu.

Mchezaji huyo mwenywe umri wa miaka 27 alitolewa nje ya uwanja katika dakika ya 87 wakati klabu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuumia wakati akiwania mpira na Fernandinho. Salah juzi Jumanne alikutana na timu ya madaktari Misri jijini Cairo kwa ajili ya kufanyiwa uchuguzi wa maumivu yake.

“Majeraha yake yanahitaji kipindi cha matibabu ili kumuwezesha kupona,” ilisema taarifa ya timu hiyo ya taifa ya Misri.

Salah alikosa mchezo wa Liverpool dhidi ya Manchester United mwezi uliopita baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Leicester, Hamza Choudhury, katika sehemu hiyo hiyo ya mguu.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, ambaye alichukizwa na rafu hiyo ya Choudhury wakati Liverpool ikishinda mabao 2-1, alisema hilo ni pigo la hivi karibuni kabisa la Salah, ambaye msimu uliopita alishirikiana na wachezaji wengine wawili kuongoza kwa mabao mengi. Liverpool mchezo ujao itacheza ugenini dhidi ya Crystal Palace utakaofanyika Novemba 23.

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amewataka mashabiki wa timu hiyo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi