loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kukodi ndege ya mizigo kupeleka maua, samaki nje

SERIKALI imesema itakodi ndege kupeleka matunda na mbogamboga nje ya nchi kutoka katika viwanja vya ndege vya Songwe na Mwanza, wakati huu ikijiandaa kununua ndege ya mizigo kwa kazi hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema). Katika swali lake, Selasini alisema Mkoa wa Kilimanjaro na hasa Wilaya ya Rombo ni wakulima wazuri wa parachichi, lakini matunda hayo yanapelekwa kwa wingi nchi jirani ya Kenya na kusafirishwa kwenda ughaibuni, kwa nini serikali isinunue ndege ya mizigo kwa kazi hiyo.

Kamwelwe alisema kwa sasa serikali inaitumia ndege ya KLM kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kubeba mazao hayo kila siku kwenda Ulaya. Alisema kutokana na hali hiyo kwa sasa serikali itatumia kukodi ndege katika viwanja vya Mwanza na Songwe kwa ajili ya kubeba minofu na mazao kama parachichi kupeleka Ulaya.

Alisema soko la bidhaa kutoka Tanzania kwenda Ulaya ni kubwa, lakini la kutoka Ulaya kuja Tanzania bado ni dogo, hivyo wataendelea kukodi wakati mpango wa kununua ndege ya mizigo ukiendelea kufanyiwa kazi.

Akijibu swali la nyongeza, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema hivi sasa serikali inaandaa sheria ya kuunda mamlaka ya kusimamia mazao ya mbogamboga na matunda ambayo itafanya kazi ya kusimamia sekta hiyo yakiwamo mazao ya parachichi. Alisema sheria itatungwa hivi karibuni ya kuwa na mamlaka hiyo, na kwa sasa baadhi ya matunda hayo yanasafirishwa kwa njia za anga na bandari kwenda nje.

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Mgaya Kingoba, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi